Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Naamini waliokuwa wakipata tabu juu yangu Ni wengi mno, manake nilikuwaga karembo bhanaaaa[emoji23] kapole Sana na kenye aibu nyingiiii, Kuna baadhi tukikutana wanataka watake advantage[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],

Mi nilimpenda mkaka flani tukiwa form 3 nae alinipenda nadhani manake alikuwa anaona sifa kweli kuwa karibu na mrembo wa shule[emoji2956][emoji2956], alikuwa anafanya poa class kunizidi nami nikaamza kukaza ili nimfikie nikampita na kumpita akaanza kunikunjia akawa anabana hata kunifundisha akaacha,, na kwa miluzi ilivyokuwa mingi nikampotezeaga, tulikutana 2015 ndipo kunitongoza nami nikamwambia nilimpendaga miaka hiyo,,, ila sio kwa utu uzimani tena, mi nikamuona km bado mdogo sana akili yangu iko mbele kuliko yake[emoji36][emoji36][emoji36] na vile nimeolewa na mwanaume mkubwa karibu nusu ya umri wangu Basi wakaka niliosoma nao nawaonaga bado wavulana
Huo ni ubinafsi tuuu
 
Nimemkumbuka Dotto Manyasi. Tulisoma Pamoja Iseni Primary School, Nyegezi Mwanza. Nilikuwa tukitoka Shule saa 8 mchana, jioni saa 10 nafunga safari mpaka kwao Nyegezi kijiweni, Naangalia nyumba yao mpaka saa 12 jioni narudi home. Moyo umefurahi kabisa.
Sikuwahi kumtamkia chochote zaidi ya kutabasamu kila tukigongana macho.
Nashukuru Mungu nilifanikiwa kupata picha yake siku ya Graduation ya la Saba. Mpaka sasa ninayo.
 
Baada tu ya kuanza form one baba alikufa kisha mama naye akafa kwa mshtuko baada ya kupata taarifa za kifo. Washikaji waliniambia baada ya ule msiba Jackie hakwenda tena shule hadi tena! Nasikia maisha yake yalivurugika sana, miaka mitatu baadaye siku moja nikiwa sokoni na mshikaji wangu mmoja akanionyesha Jackie yule pale. Dah! Alikuwa ameisha sana yaani sio yule Jackie wangu, jamaa akaniambia nimpe Hi lakini nilishindwa kwakweli. Sijawahi kumuona hadi leo.
Very emotional text, hope she make it through
 
Baada tu ya kuanza form one baba alikufa kisha mama naye akafa kwa mshtuko baada ya kupata taarifa za kifo. Washikaji waliniambia baada ya ule msiba Jackie hakwenda tena shule hadi tena! Nasikia maisha yake yalivurugika sana, miaka mitatu baadaye siku moja nikiwa sokoni na mshikaji wangu mmoja akanionyesha Jackie yule pale. Dah! Alikuwa ameisha sana yaani sio yule Jackie wangu, jamaa akaniambia nimpe Hi lakini nilishindwa kwakweli. Sijawahi kumuona hadi leo.
Mkuu Jackie alikuwa mwenyeji Wa Kahama?
 
Namkumbuka sana Mage Wa Pale Edmund rice sinon secondary Arusha. 2007-2010 form one to form 4. She was my crush ila nilikuwa domo zege. Yeye mwenyewe alikuwa ananielewa lakin sasa uoga nikikutana naye nakimbia. Alikuwa mpaka ananifata lakin naogopa kumwambia. Dah, Mage, nikikumbuka naumia sana na udomo zege wangu. Mpaka form 4 sikuwahi kumwambia kitu. Tulimaliza akabaki pale kuendelea na 5 sisi tukajiunga zetu kwa Kikwete. Nilikuja kumuona Facebook nikamcheki lakin tukawa tunachat kwa kujikongoja. Nikaamua kuvunga tu. Nilikutana naye mahali nikajaribu kuita nahisi alikuwa na mume akaogopa kusimama. Dah, Mage ulipo nakukumbuka sana.
 
Daah.joice huyu nilikuwa nampenda lakini nilikuwa namuogopa.yaani nikimuona yuleee nakimbia
 
Dah... mtoto pendo... nisipoenda class vidudu hasomi, analia siku nzima hadi arud hom anione....

Nami nikampenda, sipandi piki piki 110 ya baba adi niwe na pendo

Pendo roho iliniuma baba angu alipoamua darasa la kwanza nikasomee kwetu milimani... huo ukawa mwanzo wa kukupoteza pendo.

Ninarud darasa la3, pendo wamehama, haijulikani wapi... naangukia kwa salma... mtoto mixer mrangi na muarabu... salma anakua serious hanipendi hadi siku nawakuta wanacheza kimama mama... nakaitwa niwe baba... penzi likawa la kweli... nikitoka shule salma lazma aje kwetu... nimuoneshe mbwa wangu simba.. mbwa anayeogopeka mtaani kwetu nyuma ya mskiti wa masjid qubah.... ah salma tukicheza kombolela twaenda jificha juu ya magunia ya mahindi yalopangwa hadi juu... tunatafutwa hadi tunaitwa tujitokeze...

Tunahamia chang'ombe hadith yangu na salma nayo inaishia hapo...

Najikuta namtaman nankumpenda mtoto anjelina... ila yuko sirias na shule, hataki ujinga... ananikataa

Maisha yanaenda kwa kasi huku na kule namaliza form4... nakuwa rafiki na jamaa mmoja... urafiki kupitia rafiki.

Naenda kumpitia nyumbani kwa jamaa twende club84, lahaulaaaah... namkuta pendo... kumbe jamaa ni kaka ake pendo... pendo hanikumbuki na mm naingia ganzi coz imekua pisi kali balaaaaaaaa.

Baada ya muda namkumbusha... dah pendo anafurah... tunaanza urafiki.... baada ya muda kidume naomba game...

Pendo anakolea kwa shoo za kibabe na kisela.... lkn anakuja gundua nina pisi nyingine..... anapata tabu sana hadi jamaa ikabidi aniombe nimsaidie dada ake asije kufa kwa tatizo la moyo... mimi usela unakua mwingi nimekolea kwa mtoto wa kiswazi mtoto wa kawaida sina ilanhana complication... mtoto wa kiswazi ila anaishi kizungu..... kuhama mkoa inakua suluhisho kwa pendo... anaenda kwao moshi....

Maisha yanaenda kwa kasi ya ajabu...

Siku nipo nam hotel, nakula zangu bia, mara zinaingia pisi kama 3 ivi kali balaa... kuchek moja naiona kumbe ni salma... dahhh.... bila kujizuia kaja tukahug.... salma kachora mitatuu... salma anaonekana kawa paka shume... anaonekana ukiingia kiboya unapigwa ela na mzigo hupati... kumbe yana apointment na mbunge fulani wakale raha..

Salma ananipa namba.... baada ya kuondoka na yule mbunge... usiku salma ananichek ananiambia amelewa sana anaomba nikamchkue nmpeleke nyumbani... dah

Kiukweli sikuweza kubisha, namkuta dodoma hotel, anaingia kwe taksi ya jamaa yangu yasin mzee wa kuwalamba... jinsi alivyo jambazi kumbe salma keshanitathmini kajua labda nna maisha... dah kumbe me kachala tu mzee wa mishe mtu wa watu... akiwa amenikumbatia ananiambia hawez kwenda kulala pekeake kwanza kwao hawatamfungulia.... dah.. kidume namwambia yassin anipeleke geto.....

Mwezi na zaidi salma anakolea... mara paap... siku anakuja na kikaratas cha hospital... kapima ana mimba, yuko pia na kipimo cha mkojo kwamba kama siamini apime tena mbele yangu... lahaulaaa

Salma uyu uyu mtoto wa mjini mwenye mambo mengi... aaah siwez zaa na mwanamke wa ivi mimi... najisemea akilini

Salama anagoma kutoa mimba anaamua kuzaa..

Mishe za hapa na pale... huku na kule tunapoteana na salma...

Maisha yanaendelea...
[emoji23]
JamiiForums-223062044.gif
 
Baada tu ya kuanza form one baba alikufa kisha mama naye akafa kwa mshtuko baada ya kupata taarifa za kifo. Washikaji waliniambia baada ya ule msiba Jackie hakwenda tena shule hadi tena! Nasikia maisha yake yalivurugika sana, miaka mitatu baadaye siku moja nikiwa sokoni na mshikaji wangu mmoja akanionyesha Jackie yule pale. Dah! Alikuwa ameisha sana yaani sio yule Jackie wangu, jamaa akaniambia nimpe Hi lakini nilishindwa kwakweli. Sijawahi kumuona hadi leo.
Hee ila wanaume[emoji848]

Sasa kwanini usimsaidie?
 
😂😂 hili neno la wacha we alikua anapenda sana kulitumia bby angu yani kipindi namueleza ya moyoni navyompenda yeye anasema wacha we...usinambie!! aisee.
🤣🤣🤣🤣🤣
Na mimi ndio zangu!!
 
Mdogo wangu akiwa darasa LA 5 Kayumba primary school. Kuna mdada WAnasoma nae same class, binti akamuandikia barua ya mapenz kua anampenda. Dogo aka panic kachukua barua kaenda kumsemea kwa mwalim wa darasa ikabidi mzee aitwe shule. Mzee alirudi home a nacheka, na sisi home tukacheka Sana. Apo nipo form 3.
 
Back
Top Bottom