Okay kwanza nianze Primary 1999-2005 nilikua napendwa na mdada mmoja wa kuitwa Lucy,na mm pia nlikua nampenda ila sijui ilikua inakuaje nikimuambia nampenda yeye anakataa,ikafka mda yeye akaanza kunambia ananipenda na mm nakataa,
Kufika la Saba mwanzoni akatokea crush mwingine alikua dada wa mshkaji wangu alikua anasoma St.Anthony Mbagala alikua form two mm la saba,Damn nlimpenda yule mdada alikua msafi ananukia mda wote,nikirudi nyumbani najisemea kesho namuambia kuwa nampenda,nikimuona kesho mdomo unakua mzito,Huyu binti ilikua nikimuona moyo wangu unakua na amani sana!yani nilimpenda kweli.
O level nilimpenda binti mmoja white hivi[emoji24], nilianza kumuona stand,Nilikua nakaa Mbagala nikipita na gari Mtongani namuona ilikua form one 2006 na tulikua tunasoma shule moja,ila ile shule walikua wanatutenganisha kijinsia,(wanaume na wanawake wanasoma madarasa tofauti)
Kufika form three Mungu sio Athumani wala Mzee Mbonde tukapangwa darasa moja Damn!hisia zikazidi kuongezeka na ubaya zaidi nilikua ndo kichwa wa darasa[emoji4].Yule binti ilikua ikifka jumamosi nalaani kwa nn wikiendi haiishi ili nmuone!
Hatimaye nlimfungukia kuwa nampenda ila alinikataa kata kata kata mpaka tunamaliza o levo.