Unamkumbuka Hemed Maneti Ulaya"chiriku"?

Unamkumbuka Hemed Maneti Ulaya"chiriku"?

Maneti na Kida wote walikwenda kwa ngoma.
Kitendo cha kusema fulani alikwenda kwa ugonjwa fulani, ni kinyume cha maadili, huko ni kutoa siri za mgonjwa!. Unless wewe ni mwanafamilia, ugonjwa wa mtu ni siri ya mgonjwa, dakitari wake na familia yake!.
P
 
Kitendo cha kusema fulani alikwenda kwa ugonjwa fulani, ni kinyume cha maadili, huko ni kutoa siri za mgonjwa!. Unless wewe ni mwanafamilia, ugonjwa wa mtu ni siri ya mgonjwa, dakitari wake na familia yake!.
P
Nimekutana na Kida Waziri anamtangaza Yesu Kristo.
Ameokoka na amekuwa Mtumishi wa Mungu.
 
Alishawahi sema "Dunia aikaliki, ahera hakuendeki nimepatwa na mfadhaiko" katiki wimbo wa V.I.P, hapa naona kama alikua anadhihaki uwezo wa Mungu na Akampeleka ahera ili akakujue vizuri.!!!
 
Nionavyo mimi, VIJANA JAZZ imeuliwa na CCM yenyewe hasa baada ya TOT kuangaliwa zaidi. Album yenye wimbo shoga siyo ya mwisho kwa vionjo vya Vijana JaZz. Album ya mwisho ya Vijana Jazz kwa vionjo hasa vya wana Saga Rhumba ni ile ya 1997 ambapo majina makubwa yalikuwepo: Fred Benjamin,Suleiman Mbwembwe, Shomar Ally,Abdallah Mghonazero, Mhina Panduka( Toto Tundu) Shakashia na wengine wengi
Album hii ilikuwa na nyimbo ya Album uitwao Bye Bye Umaskini. Nyimbo zingine ni Mama Samia, Mbuzi yake Kamba nk
Baada ya Album hiyo Vijana wakapotea wakajitutumua mwaka 1999/2000 na nyimbo za Mabaar Maid, I love you mpiga debe, lakini vionjo vyake havikuwa ile dansi ya Vijana Jazz per see! Haikufanya vizuri, tangu hapo hamna Vijana Jazz, wanajaribu kuimba nyimbo za zaman lakini sauti zao hazivutii pale wanamuziki wake wanapojaribu kurudia nyimbo za zamani
Kuna siku nilienda pale Chem chem bar Tabata miaka 3-5 iliyopita, nikakuta Vijana JaZz ya kisasa wakirudia nyimbo kama:
Janja ya nyani, kapu la mjanja, shoga, VIP, Top Queen,wifi, mwisho wa mwezi, ogopa tapeli, ngapulila, visa vya mume, thereza,mfitini,bujumbura, aza, mama wa kambo, nk, nilitokwa na machozi jinsi watu wale walivyokosea kuimba nyimbo hizi tamu!
Hizo pia zaweza kuwa sababu lakini bado nafasi ya Hemedi ilikuwa kubwa kuliko Bendi.

Nikiwa bado mdogo kabisa wa shule ya Msingi uwanja wa Sheikh Amri Abeid kulikuwa na shughuli ya kiserikali (sikumbuki ni shughuli gani), nilikuwa mmoja wa Wahudhuriaji na kulikuwa na bendi...nakumbuka kuelekea mwishoni MC wa shughuli ile akatangaza wakati Bendi inaanza kutumbuiza "huyo ndio Chiriku Maneti"....nakumbuka iliibuka bonge la Shangwe na Watu waliokuwa wamezagaa wakaja kuizunguka bendi...sasa utaona kati ya Bendi na Maneti nani alikuwa na nguvu.

Uwepo wa Maneti ungeibakiza nguvu ya Bendi hata kama ingekuja TOT.
 
Back
Top Bottom