Nionavyo mimi, VIJANA JAZZ imeuliwa na CCM yenyewe hasa baada ya TOT kuangaliwa zaidi. Album yenye wimbo shoga siyo ya mwisho kwa vionjo vya Vijana JaZz. Album ya mwisho ya Vijana Jazz kwa vionjo hasa vya wana Saga Rhumba ni ile ya 1997 ambapo majina makubwa yalikuwepo: Fred Benjamin,Suleiman Mbwembwe, Shomar Ally,Abdallah Mghonazero, Mhina Panduka( Toto Tundu) Shakashia na wengine wengi
Album hii ilikuwa na nyimbo ya Album uitwao Bye Bye Umaskini. Nyimbo zingine ni Mama Samia, Mbuzi yake Kamba nk
Baada ya Album hiyo Vijana wakapotea wakajitutumua mwaka 1999/2000 na nyimbo za Mabaar Maid, I love you mpiga debe, lakini vionjo vyake havikuwa ile dansi ya Vijana Jazz per see! Haikufanya vizuri, tangu hapo hamna Vijana Jazz, wanajaribu kuimba nyimbo za zaman lakini sauti zao hazivutii pale wanamuziki wake wanapojaribu kurudia nyimbo za zamani
Kuna siku nilienda pale Chem chem bar Tabata miaka 3-5 iliyopita, nikakuta Vijana JaZz ya kisasa wakirudia nyimbo kama:
Janja ya nyani, kapu la mjanja, shoga, VIP, Top Queen,wifi, mwisho wa mwezi, ogopa tapeli, ngapulila, visa vya mume, thereza,mfitini,bujumbura, aza, mama wa kambo, nk, nilitokwa na machozi jinsi watu wale walivyokosea kuimba nyimbo hizi tamu!