Uchaguzi 2020 Unamkumbuka Kasusura? Kaka yake atia nia Biharamulo

Uchaguzi 2020 Unamkumbuka Kasusura? Kaka yake atia nia Biharamulo

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Kama unazo kumbukumbu ya jamaa mashuhuri hapa Tanzania kipindi hicho alikwapua mamilioni ya pesa na kutokomea kisha kudakwa na baadae kushinda kesi na sasa yupo kitaa baada ya kaka yake ambaye ni mwanasheria na kamishna wa jeshi la polisi akidaiwa kumsaidia kukwepa jela sasa ndio anachukua jimbo

James Kasusura mtoto wa Chief Kasusura wa kabila dogo la wasubi wa wilaya ya Biharamulo kwa aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa mkurugenzi wa Jiji la Mbeya akitokea makao makuu ya jeshi la polisi analitaka jimbo la Biharamulo ambalo baba yake alikuwa mbunge wa kwanza wa jimbo hilo na kudaiwa kumlea Rais Magufuli kama mwanae enzi hizo akisomea seminari ya Katoke.

Inadaiwa Rais Magufuli alibarikiwa na Chief Kasusura kulichukua jimbo hilo lakini alishindwa na Marehemu Kabuye na kupata baadae baada ya jimbo kugawanywa kuwa Biharamulo Magharibi na Mashariki.

Aliyekuwa mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa kwa sasa anapumulia mashine kwa kushundwa kupigania jimbo na hivyo kuna nafasi kubwa ya kamishna huyu wa polisi akitokea OCCID kuchukua nafasi kama mzawa wa Biharamulo .

USSR
FB_IMG_1595007244347.jpg
 
Hao akina Kasusura ndo wenye Biharamulo yao ni haki kuwa wabunge,wana uchungu nayo sio kama akina Mukasa waamiaji hawana uchungu kabisa na maendeleo ya Biharamulo. Biharamulo naijua vizuri.
 
Hao akina Kasusura ndo wenye Biharamulo yao ni haki kuwa wabunge,wana uchungu nayo sio kama akina Mukasa waamiaji hawana uchungu kabisa na maendeleo ya Biharamulo. Biharamulo naijua vizuri.
Mkuu nani alimpa sumu Dr. Mbasa, tetesi zinasemaje.
 
Dah umenikumbusha bwana Justin Kasusura alitingisha sana enzi zile na huo mkasa wa mamilioni aliyo toweka nayo.
 
Ikoje hiyo biharamulo

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Ni wilaya iliyo nyuma sana kimaendeleo kutokana na sababu kadha wa kadha ils kubwa ni 1. Muamko kwa wenyeji, wenyeji ni watu walio ridhika na hali zao za umasikini yaani wanafurahia maisha yao duni,ukitaka kujua watu wenye utapiamlo nenda Biharamulo.

2. Hakuna vyanzo vya kutosha vya kiuchumi/kipato hii ni kutokana hakuna zao kuu linaloeleweka linapatikana Biharamulo wankilimo mseto na ambacho ni small scale, hakuna ziwa n.k. Ngoja tuone utalii ukianza labda mambo yatakuwa vizuri labda uwekezaji kwenye utalii utainufaisha Biharamulo pia.
 
Kwao ni Kyaka Missenyi,wengine usema ni waganda kabisa sema pale kyaka kuna kabila linaitwa waganda kyaka
Kasigazi,
Bojo otabeiyha;
Kuanzia Kyaka,Igayaza, Byamutemba, Nsunga, Mutukula, Minziro, Bunazi, Nyakanyasi kuna mchanganyiko wa makabila.
Eneo lote la Misenyi ni Watanzania, ilikuwa Division ikitawaliwa na Chief Sarapioni Kyamkumwa kabla na baada ya uhuru!!
Gen Iddi Amini Dada wa Uganda alipo vamia eneo hilo, President Mwl JK Nyerere aliamuru Tz na JWTZ tuingie vitani kukomboa aridhi ya Tanzania!!
Hivyo kina Mukasa na wenyeji wa misenyi ni Watanzania halisi!!
 
Ni wilaya iliyo nyuma sana kimaendeleo kutokana na sababu kadha wa kadha ils kubwa ni 1. Muamko kwa wenyeji, wenyeji ni watu walio ridhika na hali zao za umasikini yaani wanafurahia maisha yao duni,ukitaka kujua watu wenye utapiamlo nenda Biharamulo.

2. Hakuna vyanzo vya kutosha vya kiuchumi/kipato hii ni kutokana hakuna zao kuu linaloeleweka linapatikana Biharamulo wankilimo mseto na ambacho ni small scale, hakuna ziwa n.k. Ngoja tuone utalii ukianza labda mambo yatakuwa vizuri labda uwekezaji kwenye utalii utainufaisha Biharamulo pia.
Kabisa Biharamulo na ngara ndio wilaya masikini katika mkoa wa Kagera
Ila Biharamulo imezidi ukifika nyakahula na Lusahunga kuna umasikini waliotopea
 
Kabisa Biharamulo na ngara ndio wilaya masikini katika mkoa wa Kagera
Ila Biharamulo imezidi ukifika nyakahula na Lusahunga kuna umasikini waliotopea
Lusahunga huku wapo waha na washubi
 
Kasigazi,
Bojo otabeiyha;
Kuanzia Kyaka,Igayaza, Byamutemba, Nsunga, Mutukula, Minziro, Bunazi, Nyakanyasi kuna mchanganyiko wa makabila.
Eneo lote la Misenyi ni Watanzania, ilikuwa Division ikitawaliwa na Chief Sarapioni Kyamkumwa kabla na baada ya uhuru!!
Gen Iddi Amini Dada wa Uganda alipo vamia eneo hilo, President Mwl JK Nyerere aliamuru Tz na JWTZ tuingie vitani kukomboa aridhi ya Tanzania!!
Hivyo kina Mukasa na wenyeji wa misenyi ni Watanzania halisi!!

Aho tiyabeihya; kwasababu wengi wanaoishi maeneo hayo jina maarufu waganda Kyaka
Ni wa Tanzania wenye asili ya Uganda na Wahaya mlivyo wabinafsi Mkasa hawezi kuleta maendeleo Biharamulo.
 
Back
Top Bottom