Kuna mtu anayeweza kunikumbusha ilikuwaje Babu na u-intellectual wake wote akakubali kuja kufanya siasa chini ya Mrema ndani ya NCCR-Mageuzi? Sikumbuki vyema lakini nadhani NCCR walijaribu kumfanya kuwa mgombea mwenza wa Mrema lakini ikashindikana!
Naomba nieleweke kwamba namuheshimu sana Babu na vitabu vyake navisoma sana hadi sasa. nataka tu kujua ilikuwaje akakubali kurudi kwenye siasa kupitia mlango huo!
GT,
Babu hatasahaulika just for the fact that he was an intellectual who put his intellect to work. Alijitahidi kuandika vitabu na hivi vitasaidia kuweka historia yake. Unlike Kambona ambaye aliishi Uingereza God knows kwa miaka mingapi. Alishindwa kuandika hata kitabu kimoja tu kuelezea tofauti kati yake na Nyerere. By the way Babu was also a friend so I am a bit biased.
..companero....naomba link nipate kusoma vitabu vya babu.....nimesoma mtazamo wake uliouweka hapo ./.umenipa kichaa kuona kuwa tanzania tulikuwa na watu makini kama hapa tukashindwa kuwatumia......
sijui ni lini pale chuo kikuu huwa wanapata muda wa kumjadili pof babu [kama mwanazuoni].............these heroes will soon be forgotten kama hakuna hata kitu kinachoitwa kwa majina yao...na kusoma maandiko yao,huo ni udhaifu wetu mkubwa..watanzania.
Abdulrahman Babu said:Historians will probably locate the beginning of disintegration of the regime's leadership at the February 1972 unprecedented Cabinet reshuffle, which threw out some of the most experienced ministers, including myself, (altogether, a total of about one hundred years of combined cabinet experience - a serious manpower loss to the country). In our place, were appointed some very junior and inexperienced technocrats whose only qualification for such senior appointments was their total and uncritical loyalty to President Nyerere personally. They were all 'yes-men', described by Nyerere as the 'believers', as in religion (waumini in Kiswahili).
Kuna mtu anayeweza kunikumbusha ilikuwaje Babu na u-intellectual wake wote akakubali kuja kufanya siasa chini ya Mrema ndani ya NCCR-Mageuzi? Sikumbuki vyema lakini nadhani NCCR walijaribu kumfanya kuwa mgombea mwenza wa Mrema lakini ikashindikana!
Mwawado,Mkuu Jasusi utakuwa hutendi haki kumfananisha Prof.Babu na Mzee Kambona.Wanafanana kwa sifa moja tu kwamba "wote ni waanzilishi wa Taifa letu Tukufu Tanzania",Lakini ni watu waliokuwa na mitazamo Tofauti....Wakati Babu alikuwa kada wa Mashariki,Mzee Kambona alikuwa anatazama zaidi Magharibi ya akina Kennedy kama ilivyokuwa Mwalimu Nyerere....Marehemu Nyerere alikuwa Rafiki wa Karibu wa Oscar Kambona kuliko Babu ambaye alionekana kama Mjamaa Mzanzibari.Nyerere alianza kuwa Mjamaa baada ya Ziara ya China na kuanzishwa kwa Azimio la Arusha - 1967.
Mara ya mwisho kukutana na Prof.Babu ilikuwa Harlem,New York Novemba'90 kwenye Warsha iliyoandaliwa na organization ya Malcom X (RIP) ambayo Prof. Babu alizungumza, Warsha iliyokwenda kwa Title: "Radical Tradition & a Legacy of Struggle".Mwalimu Babu alikuwa na mahusiano ya karibu na Malcom X,inaelezwa kuwa Malcom na Babu walikutana mara ya kwanza July'64 huko Cairo kwenye Uzinduzi wa O.A.U,Wakati huo Babu akifuatana na Mwalimu Nyerere,Prof. Babu akiwa Waziri ktk Jamhuri ya Muungano.Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume.
Prof.Babu alizaliwa Zanzibar na alipata Elimu yake UK ambako ndiko alikokimbilia baada ya kutoka Jela 1978/79.Katika maisha yake ya ujana Prof.alijifunza sana Ujamaa wa Mashariki,alikuwa kipenzi wa Afrika na Mwanamapinduzi wa kweli.....alishiriki katika kampeni na kumshauri Rais Nkrumah na hatimaye kushinda Urais wa Ghana 1956.
Kwa upenzi wake wa Siasa za China na Mfumo wa Ujamaa aliweza kukutana na Viongozi wakuu wa Mataifa ya kijamaa kama Mao Tse Tung,Waziri Mkuu Chou En Lai,Marshal Chen Yi na muasisi Deng Tsiao Ping.Pia aliwahi kuwa mwandishi wa kujitolea wa Chinese News Agency (HSINHUA).Ikumbukwe kuwa Ziara aliyoifanya Mwalimu Nyerere na Prof.Babu huko China ndiyo iliyomfanya Mwalimu aupende Ujamaa na kuanza kuvaa Chon en Lai (Suti za kichina),na kufuatia Ziara hiyo ndio ukaanza Mgongano wa kimtazamo kati ya Mwalimu na Mzee Kambona ambae alikuwa na mtazamo wa kimagharibi zaidi, mgongano huo ulimfanya Mzee Kambona ajiuzulu Uwaziri.
Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana,lakini ni wazi kuwa kwa tabia ya Nyerere si rahisi kukaa karibu (Zizi moja) na mtu anayemzidi akili au kuwa tishio ktk misimamo yake,na ndio maana urafiki wake na Kawawa na Munanka ulidumu kwa muda mrefu,kwa sababu waungwana hao hawakuwa challenge kwake...ni watu wa Yes Sir!! kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.Babu aliondoka Tanzania kwenda US mwaka 1978/79 baada ya kifungo...na baadaye aliondoka US kuhamia UK.
Kwa mnaotaka kuona maandiko mahiri ya Prof Babu someni kitabu kiitwacho "African Socialism" alichoandika akiwa Jela,Prof Babu atakumbukwa zaidi kwa juhudi zake binafsi kama Waziri, za mazungumzo na hatimaye Ujenzi wa Reli ya Tazara......kwa wale waliopo USA wanaweza kupata maelezo ya kuvutia yamuhusuyo Babu kwa kuzungumzana Prof Ali Mazrui (Boston) au kwenye Kumbukumbu za Malcom X,Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.
Kaka GT Shukran kwa kuleta kumbukumbu ya huyu Mwanamapinduzi!!
Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume....Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana...kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.
...Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.
Abdul Rahman Babu ndiye injinia wa siasa zilizoshindwa za ujamaa na kujitegemea na zile za vijiji vya ujamaa Tanzania.
Nyerere alikuwa haujui ujamaa wa kikomunisti maana shule zote alizosoma Nyerere zilikuwa za kikatoliki na vyuo alivyosoma vyote ukomunisti haukuwemo kwenye mtaala wa masomo yake.
Kilichotokea ni kuwa alipata mori wa Tanganyika ipate uhuru ijitawale.Ila nadhani hakujua vizuri ikipata uhuru iende kwa siasa ipi? Ndiyo maana miaka ya mwanzo ya uhuru huoni Nyerere akitamka kuwa Tanzania itakuwa ni nchi ya yenye kufuata siasa ipi zaidi ya porojo.
Sasa baada ya Tanzania kuungana na Zanzibar alimchukua Mzanzibari Abdulhaman babu na kumpa uwaziri wa mipango ya uchumi ya nchi.Alipopewa ndipo akaanza kuandika kwenye gazeti la Nationalist la Tanzania kuhusu mawazo yake ya siasa za ujamaa na kujitegemea.
Hapo ndipo akaanza kumfundisha Nyerere kuhusu ukomunisti na ujamaa ambao kwa Nyerere lilikuwa somo jipya ambalo hajawahi kulisikia wala kulifanyia mazoezi na mtihani lakini linalovutia kusikiliza.Na kwa sababu Nyerere alikuwa msomi akamwamini sana msomi mwenzie Babu kwa vile alivyokuwa akisema vyaweza leta faida.Na ni kipindi hicho hicho ndipo na Nyerere naye alipojifanya kinara wa ujamaa kwa kuanza kuandika vitabu kama FREEDOM AND SOCIALISM akiandikia ujamaa anaouita wa Kiafrika (AFRICAN SOCIALISM) ambao haujawahi fanyiwa majaribio popote katika Afrika yeye akaanza kujifanya Nabii mwafrika mwanzilishi wa huo ujamaa koko! Na msemaji wake maarufu na akaamua Tanzania ndiyo iwe nchi ya kuanzia ya kujaribishia huo ujamaa ambao haujawahi kuwepo.
Nyerere akazidi kumwamini Babu akamwachia injinia huyo wa siasa ya ujamaa zilizoshindwa kabla ya kuanza ajaribu hayo mawazo yake ya kindoto kwenye mipango ya uchumi ya Tanzania kama waziri.
Siasa ya ujamaa ikaingizwa na kutangazwa kama sera ya nchi na siasa ya kufuatwa na nchi kipindi hicho cha Babu alipokuwa waziri.Marafiki zetu wakaanza kuwa wachina,warusi,wakorea na wa-cuba ambao ndio waliokuwa walimu wakuu na viranja kwenye shule na seminar alizoenda Babu ambao Babu alikuwa akinukuu mawazo yao kwa kila akisemacho na aandikacho.
Walichokosana na Nyerere ni kuwa baada ya kumwamini Babu na mawazo yake ya ujamaa slikuja kuona hayasaidii nchi kwenda mbele na hayatekeleki kuanzia vijiji vya ujamaa,maduka ya ushirika,Azimio la Arusha n.k kuonekana vinadorora
Nyerere alianza kumwona Babu kama tapeli wa kisiasa aliyemchuuza mchana kweupe na kuua umaarufu wake ili aonekane hafai mbele za wananchi kwa kumshauri vibaya kama waziri aliyemwamini.Akaona kila kilichozalishwa na Babu kwenye siasa za nchi hii kinakufa magotini kwake .Akaamua kumtema Babu na kuachana naye kwa hasira za kizanaki zilizochanganyika na za kikurya za kwa wajomba zake.
Akaachana naye kimya kimya na kumzira.Naye Babu akaondoka kwenda kufundisha na kuandika kuhusu huo ujamaa wake ambao haukuwa na mahali pa kuufanyia kazi zaidi ya madarasani na kwenye midahalo ya wasomi kwenye kuta za vyuo vikuu ya mashindano ya maneno yasiyo na vitendo vya kusaidia wananchi.Huko ndiko mtu maarufu lakini kwa mtanzania jamaa alitutia umaskini na sera zake huko wizara ya mipango alikokuwa.
Tunachojifunza ni kuwa Mtu anapotaka kuwa Raisi ni vizuri yeye mwenyewe ajue atafuata siasa au njia ipi...
Tusiandikie mate wakati wino upo na wino ndio maelezo haya ya Babu mwenyewe kutoka kwenye huo Muswada wa Kitabu alichokuwa akiandike kuelezea nini hasa kilitokea kati yake na Mwalimu:
Kwa kuwa hicho kitabu chenyewe cha Babu hakijachapishwa bado hayo ni mate na siyo wino.
... na Nyerere alikuwa very interested na kichwa hiki - Abraham Babu..
... Nyerere alijua kwamba anamhitaji Abraham Babu na vichwa vingine toka visiwani akawavuta bara kama serikali ya Muungano kwa maslahi ya bara..