Unamkumbuka Mussa Simba aka Black Moses: Huyu alikuwa bingwa wa Disco miaka hiyo

Usimsahau nigger j enzi hizo,ambae ndio huyu masoud masoud,chini ya usimamizi wa the late choggo sly
Hahaha, umenikumbusha mbali.

Kuna mtu alikuwa anaitwa "Super Ngedere". Pia Ommy Sidney, Fast Eddie.
 
Unga mbaya sana huyu dogo alifikia hatua mbaya sana ,ukiacha kitu vibaya usawa wake anapita nacho.

Mpaka akawa anafungiwa ndani .
 
Reactions: T11

 
Huyo Fatuma siyo yule dada aliyekuwa mwanafunzi wa sekondari fulani mwaka 1985 au 1986 na akashinda shindano moja kubwa la kucheza break dance? Kama ndiyo yeye nakumbuka baba yake alikuwa ni baharia na baada ya kupata ushindi wa kucheza break dance na kusakamwa shuleni na mtaani kwao aliamua kujiua na kuacha simanzi kubwa. Miaka hiyo kwa Dar nilizoea kuwaona akina Black Moses na wengineo waliokwishatajwa. Pia nikienda zangu Mwanza nilikuwa nikiwaona wacheza break dance kama Bob Sado (si riziki?), Matongo (kama nimepatia jina), vijana fulani watoto wa mzee Jumbe (mmoja wa wazee maarufu pale Mwanza kwa miaka hiyo) akiishi mtaa wa aidha Rufiji au Uhuru. Enzi hizo ma Dj maarufu kwa Mwanza walikuwa ni Dj Yusuph na Bush Doctor ambao wote kwa sasa ni marehemu.
 
Dah, kujiua enzi hizo ilikuwa kama fashion...issue ndogo tu vijana walikuwa wanameza chloroquine
 
Walikuwa na uwezo kujinyonga kama nyoka. Hata mazoezi yao hayakuwa ya kitoto. Leo huwapati wa jinsi hiyo.
 
Huyo jamaa alikuwa maarufu Sana enzi hizo tukiwa wadogo.
Alifahamika Tanzania kote kupitia show zake na kuandikwa kwenye magazeti na kutajwa Radio Tanzania back then.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…