Unamkumbuka Mwalimu wako aliyekufundisha Elimu ya Awali?

Kilimbatzz

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2023
Posts
9,134
Reaction score
14,593
Mimi namkumbuka Mwl. Minja.

Yule mama Mungu ampe maisha marefu, kuna siku moja nilitaka kujisaidia haja ndogo ila zipu ya mkaputura wangu ukagoma kushuka chini!

Yule mama aliponiona nalia kwa kuhofia nitajikojolea akaja akanituliza kwanza. Akaniuliza shida nini, nikamwambia zipu imegoma kushuka chini hivyo muda wowote nalimwaga kojo.

Hakunisema wala kunipiga, ila alifungua zipu yangu na kuishusha chini kisha akakishika kibamia changu akakielekezea kwenye shimo moja ndani ya Darasa la kwanza pale Makurumla Primary School mwaka 1995, sitamsahau kwa hilo.

Popote ulipo mama Mungu akubariki.


 
Mwl Njogopa, popote ulipo Madame, ubarikiwe sanaa, sitasahau nilikua naumwa ulitandika khanga yako nilale chini.

Ulikua unanambia nna kichwa chepesii, nna kariri vitu kwa haraka, afu sisahau, ulinitabiria nitafika mbali, ile taaluma yako ulitakaga niwe nayo, niliitoa nilipofika 4m 3. niko na taaluma nyingine.

Ulihama nikiwa std 3, sijawahi kukuona tenaa. Natamani nikuone nikupe zawadi, ule msingi uliojenga kwangu ni mkubwa mnoo.

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mkwaji Nyandege, Godfrey Mkala Stephen Liso (Msosi Mniji) na madame mmoja hivi kwa sasa ni marehemu. Walinitendea mema sana.
 
Njogopa jina zuriii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…