Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mke uliyemtolea mahari na kukabidhiwa na wazazi wake. Amekuzalia watoto, anafua na kupiga pasi nguo zako, anapika chakula watoto wako na wewe hamlali na njaa leo unampa mateso haya.
Leo amekwenda saloon kusuka yeboyebo ingawa hupendi ajichanganye ili asisikie ufuska wako. Amekutana na ule mchepuko wako wa bank uluimletea kitenge ulipoenda Ivory Coast. Kumbe ulinunua sare na mke wako.
Mchepuko anamjua mke wako na anamdharau kwakua ni mama wa nyumbani. Bank ajira yake aliipata kwakua branch manager ni mshirika wako wa biashara ulihakikisha anapita usaili.
Kuna kitu unakitafuta na utakipata hivi karibuni.