Nilianza kumfuatilia AY tangu alipokuwa CBM Crew; miaka kadhaa iliyopita very certain wakati Diamond akiwa bado Primary School! Hakuna shaka kwamba kwa kipindi chote hicho AY hajasahaulika lakini sikumbuki kipindi chochote over the entire time AY alipata kuwa Top....kwenye soka ya Tanzania, AY ni kama Kagera Sugar; imeendelea kusumbua kwa kipindi chote lakini haijapata kuwa Top! Katika hili la kuwa Top, AY hajawahi kufikia hata status ya Mr. Blue!! Diamond, kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, tangu aingieze nyimbo "Nenda Kamwambie", bado hajawahi kushuka....ameendelea kuwa Top over the entire period of time; for almost Three Years Now!!
Tukirudi kwenye mafanikio, sijui tunataka kuzungumzia mafanikio ya nini....ikiwa ni ya kimuziki, angalau kwa kumlinganiasha na AY, Diamond mwacheni aitwe Diamond....the guy he's far better than AY. Hawa wote ni watu wa kujifagilia, AY huyu huyu alitutangazia kwamba kwamba ametengeneza Video kwa TZS 32 million! Lakini ukiangalia kwa makini ile video, mtu unaweza kujiuliza 32 million zilitumika tumika vipi; kwani ukiiangalia video yenyewe yenyewe, hakuna scenes zozote ambazo zinaonekana ni expensive scenes.....sana sana kuna scene za watu kula pombe!! Angalau Diamond, akisema alitumia USD 30,000 kwenye video yake, ukiiangalia video husika, inaleta sense!
Kubwa ambalo naona AY kamzidi Diamond kwa mbali ni ku-settle! AY ame-settle probably than any other Bongo Flavor Artist in TZ! Ni mtu ambae anaziona opportunities na kuzifanyia kazi. Kama mafanikio ya kimuziki ya Diamond angekuwa ndo aliyonayo AY, basi leo hii AY angekuwa kitu kingine kwa mafanikio ya kiuchumi!