Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Stv Mkn

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
328
Reaction score
273
Ndugu zangu katika kupambana na maisha kijana mwenzenu hatimaye nimepata IST na nimekamilisha taratibu zote za kuanza kufanya kazi ya Uber na Bolt. Gari ni yangu japo si mpya sana ila bado nzima kabisa nimefunga na AC.

Sasa kwa kuwa ndio naanza najua kuna mengi natakiwa kujifunza. Ningeomba madereva wazoefu mnisaidie uzoefu wenu kuhusu changamoto, fursa, utegaji mingo, malipo au lolote unafikiri linaweza nisaidia.
Pia vitu vya kuepuka nikiwa kazini.

Natanguliza shukrani. Nayeyuka!
 
Wahi kuamka alfajiri, lala mchana kisha rudi mzigoni saa kumi jioni. Uwe mstaarabu, usikose chenji na zingatia alama za usalama barabarani.

Usiwe na tamaa maana kuna wadada wengi wanakuwa na mitego ili wasilipe nauli mkifika mwisho wa safari.
Asante mkuu kwa ushauri. Jioni saa 10 mpaka saa ngapi kwa weekdays na weekends?
 
Back
Top Bottom