Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Kuna mzigo mtaani unaitwa Zuzu hiyo ni app ya kuchezesha hizo app zao zikuletee wateja unaweza ukawa k/koo msimbaz lakini uka cover mpak posta mpaka buguruni kigogo yani ukachukua large area mtu akirequest anakupata wewe kwanza hata akiwa mbali vp ila awe kwenye hizo location ambazo umezichagua na hiyo app ndo huwa inafanya michezo michafu ya kuongeza ruti ukiongeza ruti automatic na bei inaongezeka na mteja analipa hata kama bei ya mwanzo haikusoma hiyo ambayo umeingeza wakikugundua bolt wenyew wanakupiga burn ya wiki kadhaa wakikufungulia ukiendeleza michezo yako unakula burn ya milele
 
Ndugu zangu katika kupambana na maisha kijana mwenzenu hatimaye nimepata IST na nimekamilisha taratibu zote za kuanza kufanya kazi ya Uber na Bolt. Gari ni yangu japo si mpya sana ila bado nzima kabisa nimefunga na AC.

Sasa kwa kuwa ndio naanza najua kuna mengi natakiwa kujifunza. Ningeomba madereva wazoefu mnisaidie uzoefu wenu kuhusu changamoto, fursa, utegaji mingo, malipo au lolote unafikiri linaweza nisaidia.
Pia vitu vya kuepuka nikiwa kazini.

Natanguliza shukrani. Nayeyuka!
kuwa na chenji za kutosha, usipandishe walevi na kuwa na kasilaha hata kanyundo kwa ajili ya night kali
 
Back
Top Bottom