Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Unanishauri nini mimi dereva ninaeanza kuendesha Uber na Bolt?

Kwanini Hailipi? Na je unaendelea kuifanya au umeshaacha?
Nini sababu za kusema hailipi? Umetumia vigezo gani ? Na je umejifunza Nini? Na Kipi unakosea/umekosea labda ungependa yeyote anayetaka kufanya Ajifunze Nini kwanza?...

Tunaomba msaada....
Nasema hailipi sababu maybe ya expectations zangu before na vile watu walinieleza.
Kwa sasa naifanya zaidi weekend sababu ndio walau kuna pesa. Ila siku za kawaida naweza choma mafuta baadae nikilaza gari nakuta nilichopata kinarudi kujaza mafuta ya kesho so ni kama naifanyia kazi bolt. Alafu kingine mimi nakaa nje ya mji so safari ya kufika eneo la wateja wengi unakuta nishachoma mafuta ya buku 10 nikizunguka kidogo taa inaanza kuwaka inanidai wese.
Hapo sijaweka akiba ya service na pesa ya kurudisha bolt.

Nilichojifunza ni bolt inataka hesabu usifanye tu lazima ujue kwenye kila pesa mfano buku 10 kuna pesa yako pesa ya kuhudumia gari na pesa ya bolt. Ukiweza kutegua huo mtego unaweza ona faida. Na faida haiwezi kuwa kubwa sana sana kwenye elfu 10 ya kwako ni buku 3 maximum.
 
Habari zenu!

Natafuta Bajaji ya kufanyia kazi. Nipo tayari kwa mkataba au kawaida kuleta hesabu kwa siku. Nina uzoefu pamoja na uaminifu wa hali juu.

Nina Leseni na kitambulisho cha taifa (NIDA)
Namba: 0674074563
Nipo tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwa Dar es Salaam.
Nipo Dar es Salaam
 
Yani humu ukitaka ushauri unatakiwa uwe na moyo wa uvumilivu aisee lasivyo....
 
We mdau aliekurekebishia mchongo wote hauna namba yake tufanye kazi.
njoo in box siple tu ila kunauwezekano wa kustukiwa mf noah uipe cc chini ya 1500 gari ambazo sio comon au wasikague sana wawe wanasoma tu
 
Nipe headline ya uzi husika nikautafute mkuu.
[emoji116]
Screenshot_20230915-193045.jpg
 
Ofisi za bolt zipo mikocheni mtaa wa maji maji.Njia rahisi ni Ile ya viwandani ukitokea rose garden ama Kwa Nyerere ndo unaupata mtaa wa maji maji Ila now day's hii kazi imekuwa ni ngumu hasa Kwa wenye magari makato ni makubwa halafu nauli ni ndogo mafuta yamepanda bei na abiria anataka kiyoyozi.Sehemu ambazo ukienda na abiria unachoma mafuta kurudi ni njia ya kimara,Mbezi Magufuli stand.Tabata yote kule wamezoea vibajaji na boda boda.Huko wamezoea vibajaji na boda.Gari inachoka pesa ya matengezo hamna.Watu Wanafanya hii kazi Kwa kuwa hamna kazi labda uwe na gesi hapo ndo hutowaza.
 
Back
Top Bottom