Angalia gharama za mafuta za kwenda na kurudi kisha piga gharama za nauli ya ndege kwenda na kurudi,jumlisha ukiendesha uchovu na service ya gari kabla hujaanza safari,, mfano kwenda Mwanza na LANDCRUISER Vx Diesel engine ni laki 3 mafuta kwenda tu na ni masaa karibia 13 njiani na ni km 1100 hivi kutoka dar,,sasa ukipiga na nauli ya ndege bombardier haizidi laki 2 na ni kama masaa mawili hivi,,na FASTJETS ukikata mapema unapata mpaka laki 1 na nusu mpaka mwanza kwa lisaa limoja na dk 15,, kwahiyo unakuja kuona kusafiri kwa gari kutoka dar to mwanza ni gharama kubwa kuliko ndege,, maana kwa mafuta ya gari tu ya kutoka dar kwenda Mwanza unaweza kukata tuketi ya kwenda na kurudi dar,, hapo bado hujapiga gharama za service na uchovu barabarani,,nakushauri piga hesabu zako mapema kabla ya safari kwanza maana kwakweli ni umbali mrefu sana huo,,mimi huwa nasafiri dar to musoma kwahiyo naelewa umbali huo