Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UNANYIMWA MAJI KISHA UNALAUMIWA KWA UCHAFU WA KUTOKUOGA
Vita Vya Pili Vya Dunia Manazi wa Kijerumani waliwakusanya Wayahudi katika Ghetto Poland hawana maji wala vyoo.
Kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.
Jamii moja inanyimwa elimu na matokeo yake jamii hiyo inakuwa masikini.
Jamii hii inajitahidi kujinasua katika hali ile ile ya kimasikini lakini ni wazi katika umasikini huwezi kukidhi viwango kwani viwango vinahitaji fedha.
Juhudi za masikini hawa zinawekewa vikwazo kwa kutakiwa kufanya mambo kwa vigezo vya matajiri.
Ndugu yangu Muislam iangalie video hii hadi mwisho kuna funzo kubwa ndani yake.
Vijana wa Kiislam wanarudishwa makwao ili kuwaepusha na hali duni wanayoishi hapo msikitini.
Wanarejeshwa makwao kwenye nyumba nzuri zenye umeme, maji na vyoo vya kuvuta vinavyotiririka maji muda wote.
Vitu wasivyokuwanavyo.
Wanarudishwa makwao wakaishi kwa starehe na kula vyakula vizuri ambavyo havipikwi kwenye kuni na mafiga kama hayo wanayopikia hapo msikitini.
Unaweza ukacheka kwani hakika haya ni maskhara.
Hiyo Qur'an na Uislam ambao wazazi wao wamewapeleka kusoma hapo masomo hayo yasubiri kwanza hadi msikiti utakapokuwa na mabweni yenye vitanda na magodoro mazuri na vyakula kupikwa katika majiko ya umeme au gesi.
Nani asiyejua maisha ya familia wanazotoka watoto hawa?
Kuna tofauti kati ya maisha yao hapo msikitini na huko nyumbani kwao wanakorejeshwa?
Kisa cha Manazi na Wajerumani katika Ghetto za Poland Vita Vya Pili Vya Dunia.
View: https://youtu.be/eYUPhm8guek?si=-ghapT0p9jxB7Mxh