Unanyimwa Maji Kisha Unalaumiwa Kwa Uchafu

Unanyimwa Maji Kisha Unalaumiwa Kwa Uchafu

Grahams,
Tazama video na angalia DC anawauliza wamafunzi hao wamesoma hadi darasa la ngapi.

Hakuna mtoto wa miaka 3 au 8 hapo.
Usiwe na papara ya kuandika.

Elewa kwanza ndiyo uje hapa ujibizane na mimi.
Mkuu Sina uwezo wa kuendelea kubishana wakati tayari umeshachagua upande...

Unaamini hicho kilichofanyika hapo dhidi ya Waislamu wenzako ni uonevu.

Lakini swali la kujiuliza, ingekuwa ni watoto wako wa kuwazaa ungeruhusu wakakae kwenye mazingira yale na kupewa aina hiyo ya maarifa?
 
Mzee kuna kitu unajitahidi sana kukitengeneza. Hata hivyo hivyo tunawashukuru Watanganyika hawako tayari kwa hicho
 
Mkuu Sina uwezo wa kuendelea kubishana wakati tayari umeshachagua upande...

Unaamini hicho kilichofanyika hapo dhidi ya Waislamu wenzako ni uonevu.

Lakini swali la kujiuliza, ingekuwa ni watoto wako wa kuwazaa ungeruhusu wakakae kwenye mazingira yale na kupewa aina hiyo ya maarifa?
Grahams,
Unadhani hawa watoto wanatoka kwenye mazingira bora kuliko hayo ya hapo msikitini?

Watoto hawa wameulizwa na DC na wamemueleza kuwa wao wameletwa na wazazi wao na wengi wameishia darasa la saba.

DC na Kamati ya Usalama wanaweza kuwa na uchungu wa hawa watoto kuwashinda baba na mama zao?
 
Ni mjinga ndo anaweza kutetea ujinga unaofanywa na huyu sheikh.....unakusanya watoto 96 bila kuwa na mazingira wezeshi na rafiki?
 
Hii dakika ya mwisho unakuta wanaingiliana kinyume na maumbile tunazalisha mashoga.
 
Covid,
Mbona shule hiyo hapo chini haijavamiwa usiku na manane na kufungwa?

View attachment 3038995
Mkuu wa Wilaya hajapinga watoto kufunzwa mambo ya dini.Anachopinga ni kuwalaza watoto katika eneo ambalo sio salama kiusalama na kiafya. Sidhani kama atakuwa na tatizo kama hao watoto watakuwa wanaenda kulala sehemu nyingine baada ya mafunzo yao. Angekuwa ana matatizo na mafunzo ya hapo mahali asingesema kuwa warudi mabweni yatakapokamilika.

Hayo madarasa ya shule ya msingi Mlevo hayatumiki kulaza wanafunzi. Unaweza kuwafundisha watoto chini ya mti lakini ukianza kuwalaza chini ya huo huo mti utachukuliwa hatua.

Sio sahihi na haki kusema kuwa hawa watoto wanatokea katika mazingira duni basi wanastahili kulazwa katika sehemu ambayo inafanana na wanapofugiwa mifugo. Kwanza, pamoja na umasikini wao hamna ambae analazwa pamoja na watoto thelathini wenzake ambao hajui wanakotoka. Kitendo cha kuwalaza hivyo kunaweza kusababisha usambaaji wa magonjwa, vifo vingi pakitokea kitu cha dharura kama moto au hata nyoka ( vifo vingi viatokana na msongamano wa watu wanaotaka kujisalimisha na sio tukio lenyewe).

Mwisho, tunajua watoto wengi hawapati chakula cha kutosha majumbani kwao. Kwa argument yako kuwa hata huko wanakotoka maisha yao hayatofautiani na hapo panapolalamimikiwa basi ina maana hapa napo wakinyimwa chakula ( sisemi kuwa wananyimwa) ni sawa tu!

Mimi nilitegemea ungemkemea muislamu mwenzako kwa kuhatarisha uhai wa watoto wa kiislamu kwa kuwalaza katika mazingira hatarishi. Ningetegemea ungehamasisha watu wachangie kwa hali na mali ili mabweni yenye huduma zinazokubalika yakamilike mapema iwezekanavyo.

Mfano wako wa Ghetto ya Warsaw sio sahihi. Hakuna muislamu anaezuiwa kupata elimu anayoitaka. Kinachozuiwa ni kuhatarisha maisha ya hao waislamu. Naamini hata angekuwa padiri anafanya hivi, angekemewa na kupigwa marufuku. Tusigeuze kila kitu kuwa suala la udini. Uhai hauna dini.

Amandla...
 
Det...
DC kawauliza wanafunzi wanasoma kitu gani?
Wanafunzi wamemjibu, ''Qur'an.''
then wote wametoka makwao, wameacha familia zao wasome Qur’an?
Grahams,
Unadhani hawa watoto wanatoka kwenye mazingira bora kuliko hayo ya hapo msikitini?

Watoto hawa wameulizwa na DC na wamemueleza kuwa wao wameletwa na wazazi wao na wengi wameishia darasa la saba.

DC na Kamati ya Usalama wanaweza kuwa na uchungu wa hawa watoto kuwashinda baba na mama zao?
japokuwa umemjibu huyo bwana, watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu huwa wanapelekwa kwenye vituo ambavyo vinatambulika na serikal kuwa vinafanya kazi hiyo.
Huo ni msikiti, kwa sheria ya nchi inaruhusu kufanyika hayo?
Na katika umri huo , elimu dunia au elimu ipi ndio kipao mbele kwa vijana wadogo? Wangetakiwa wawe shule sahizi, hapo wanafanya nn?
 
Mas...
''Sio kila mwenye Taarifa ana Maarifa na Wala si kila mwenye Maarifa ana Taarifa.Kupata Maarifa lazima uwe na Taarifa na kupata Taarifa lazima Uwe na Maarifa.Kujua kuwa hujui ndio kujua kwenyewe.''

Unaijua shule hiyo hapo chini?:
View attachment 3039000
Nafikiri Naisikia TU.Hata hivyo tukubali tu kwamba Mazingira ya Kuishi na kulala Msikitini kwa muda mrefu Bil kuwa na Hostel Maalum zenye Ha
 
UNANYIMWA MAJI KISHA UNALAUMIWA KWA UCHAFU WA KUTOKUOGA

Vita Vya Pili Vya Dunia Manazi wa Kijerumani waliwakusanya Wayahudi katika Ghetto Poland hawana maji wala vyoo.

Kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.

Jamii moja inanyimwa elimu na matokeo yake jamii hiyo inakuwa masikini.

Jamii hii inajitahidi kujinasua katika hali ile ile ya kimasikini lakini ni wazi katika umasikini huwezi kukidhi viwango kwani viwango vinahitaji fedha.

Juhudi za masikini hawa zinawekewa vikwazo kwa kutakiwa kufanya mambo kwa vigezo vya matajiri.

Ndugu yangu Muislam iangalie video hii hadi mwisho kuna funzo kubwa ndani yake.

Vijana wa Kiislam wanarudishwa makwao ili kuwaepusha na hali duni wanayoishi hapo msikitini.

Wanarejeshwa makwao kwenye nyumba nzuri zenye umeme, maji na vyoo vya kuvuta vinavyotiririka maji muda wote.

Vitu wasivyokuwanavyo.

Wanarudishwa makwao wakaishi kwa starehe na kula vyakula vizuri ambavyo havipikwi kwenye kuni na mafiga kama hayo wanayopikia hapo msikitini.

Unaweza ukacheka kwani hakika haya ni maskhara.

Hiyo Qur'an na Uislam ambao wazazi wao wamewapeleka kusoma hapo masomo hayo yasubiri kwanza hadi msikiti utakapokuwa na mabweni yenye vitanda na magodoro mazuri na vyakula kupikwa katika majiko ya umeme au gesi.

Nani asiyejua maisha ya familia wanazotoka watoto hawa?

Kuna tofauti kati ya maisha yao hapo msikitini na huko nyumbani kwao wanakorejeshwa?

Kisa cha Manazi na Wajerumani katika Ghetto za Poland Vita Vya Pili Vya Dunia.

View: https://youtu.be/eYUPhm8guek?si=-ghapT0p9jxB7Mxh

MNAFUNDISHA WATOTO UGAIDI MNASINGIZIA DINI!SHAME ON YOU ALL!
 
Ila Mkuu wa Wilaya nimempenda bure, ameendesha zoezi lile kwa weledi wa juu sana, kiasi nampa maua aliyempa uDC.
 
UNANYIMWA MAJI KISHA UNALAUMIWA KWA UCHAFU WA KUTOKUOGA

Vita Vya Pili Vya Dunia Manazi wa Kijerumani waliwakusanya Wayahudi katika Ghetto Poland hawana maji wala vyoo.

Kisha wakawa wanawalaumu kwa uchafu.

Jamii moja inanyimwa elimu na matokeo yake jamii hiyo inakuwa masikini.

Jamii hii inajitahidi kujinasua katika hali ile ile ya kimasikini lakini ni wazi katika umasikini huwezi kukidhi viwango kwani viwango vinahitaji fedha.

Juhudi za masikini hawa zinawekewa vikwazo kwa kutakiwa kufanya mambo kwa vigezo vya matajiri.

Ndugu yangu Muislam iangalie video hii hadi mwisho kuna funzo kubwa ndani yake.

Vijana wa Kiislam wanarudishwa makwao ili kuwaepusha na hali duni wanayoishi hapo msikitini.

Wanarejeshwa makwao kwenye nyumba nzuri zenye umeme, maji na vyoo vya kuvuta vinavyotiririka maji muda wote.

Vitu wasivyokuwanavyo.

Wanarudishwa makwao wakaishi kwa starehe na kula vyakula vizuri ambavyo havipikwi kwenye kuni na mafiga kama hayo wanayopikia hapo msikitini.

Unaweza ukacheka kwani hakika haya ni maskhara.

Hiyo Qur'an na Uislam ambao wazazi wao wamewapeleka kusoma hapo masomo hayo yasubiri kwanza hadi msikiti utakapokuwa na mabweni yenye vitanda na magodoro mazuri na vyakula kupikwa katika majiko ya umeme au gesi.

Nani asiyejua maisha ya familia wanazotoka watoto hawa?

Kuna tofauti kati ya maisha yao hapo msikitini na huko nyumbani kwao wanakorejeshwa?

Kisa cha Manazi na Wajerumani katika Ghetto za Poland Vita Vya Pili Vya Dunia.

View: https://youtu.be/eYUPhm8guek?si=-ghapT0p9jxB7Mxh

Imani Yako inakufanya kama hujaenda shule hivi kweli kwa mazingira hayo mtoto wako ungeweza kum dump! Mbona DC kaeleza vizuri na utaratibu!
 
Aliekutuma uyaandike haya itabidi tumjue .. inawezekana upo kwenye payroll ya magaidi mnapewa pesa kutetea matendo ya namna hiyo
 
Back
Top Bottom