Ofisi nyingi za serikali za mitaa ama labda zote Nchini Tanzania hazina vyoo (Naweza kuthibitisha), Hii maana yake ni kwamba Wenyeviti waliopo na wananchi wanaopata huduma kwenye ofisi hizo wanajisaidia vichakanii na kusababisha uchafu na uharibifu wa Mazingira.
Kushindwa kujenga Vyoo kwenye ofisi hizo ambazo ndio sehemu yao ya kazi za kila siku, ni kushindwa kuwajibika kwa viongozi waliopo na kimsingi ni kushindwa kazi , ukichanganya na rushwa kwa wale wanaotaka barua za Utambulisho pamoja kuuzwa kiholela kwa Maeneo ya Wazi, Watu hawa hawapaswi kupewa dhamana hii tena.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ndio Kodineta wa kampeni zote za Usafi kwenye eneo lake, Zikiwemo kampeni za kutokomeza Kipindupindu, Hawa ambao wanashindwa hata kujenga vyoo vya matundu mawili watawezaje kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko?
View attachment 3124762
Ndugu Mwananchi hii ni nafasi yako ya kuondoa Uvundo wa mikojo na kinyesi mtaani kwako, kwa kuchagua viongozi makini kutoka Chadema, Wapigie kura Wagombea wa Chadema na Uilinde kura yako.
View attachment 3124757
Hii ni Kwa sababu,
MATATIZO HAYAWEZI KUMALIZWA KWA KUTUMIA AKILI ZILE ZILE ZA WATU WALEWALE WALIOYALETA
Chagua Chadema kwa ajili ya Heshima ya Kijiji Chako