Asante Philipo, yani nikimaliza tiles nitashusha pumzi kidogo maana nilihamia kwenye nyumba bila tiles huu mwaka wa pili. Lakini tuliishi na wanangu kwa Amani Sana, Jana nimeleta tiles mwanangu mmoja mdogo umri 2+ akauliza baba umeleta keki tule! fungua box tuone humo kuna nini!! kijana wangu umri 5+ akamwambia tiles hizo zimeingia, dah machozi yalinilenga lenga nikajikaza kiume, wanangu nao sasa wakanyage kioo cha tiles namshukuru Mungu Sana.
View attachment 2017441
Sent from my Redmi Note 3 using
JamiiForums mobile app