Unapataje hesabu ya kumlipa fundi tiles?

Unapataje hesabu ya kumlipa fundi tiles?

Fundi inaonyesha wewe ni fundi wa mitaa ile kule baharini.. Hapo tu nadhanj unepitiwa ila najua ulitaka kutuwekea bei in terms of Dollar.

Mimi sikuwezi kwakweli...
Hiyo ni bei halisi mkuu na mimi siyo fundi. Hiyo ni materials na ufundi ila kama ufundi peke yake huwa ni 5000/- per sqm.
 
Asante Philipo, yani nikimaliza tiles nitashusha pumzi kidogo maana nilihamia kwenye nyumba bila tiles huu mwaka wa pili. Lakini tuliishi na wanangu kwa Amani Sana, Jana nimeleta tiles mwanangu mmoja mdogo umri 2+ akauliza baba umeleta keki tule! fungua box tuone humo kuna nini!! kijana wangu umri 5+ akamwambia tiles hizo zimeingia, dah machozi yalinilenga lenga nikajikaza kiume, wanangu nao sasa wakanyage kioo cha tiles namshukuru Mungu Sana.View attachment 2017441

Sent from my Redmi Note 3 using JamiiForums mobile app
Hizo tiles za juu zisimamishe kama za chini.Pia hakikisha fundi anajua kuweka level
 
Natumae mleta mada ulipata muongozo...
Tena muongozo uliotukuka kabisa, naendelea kujifunza mengi kwenye finishing siyo mchezo, ila mafundi wengi ni madalali, anachukua kazi kwa mbwembwe kwamba anajua kupiga tiles kumbe hamna kitu, matokeo yake analeta fundi tiles na yeye anabaki kuzugazuga tu.
 
5,000 kwa Square metre ni bei standard kwa mtaani.Ikizidi sana ni 6,000.Zaidi ya hapo atakuwa ni dalali anayetaka kuuza kazi
Umesema sahihi mkuu mwambie aende kwenye magorofa makubwa wachina wanauza sqm mpk 4000 lkn anakufanyia level yeye kwahio km ulivyosema elfu 5 ni bei standard sana ikizidi elfu 6
 
Hapo kwenye bati na mbao ni zoezi ngumu sana kwa sababu pesa inahitajika kwa wakati mmoja, ndio maana wengi wakimaliza kupiga bati wanapiga kapicha mjengo nduki.Humuoni tena site anakuwa katoboka mfukoni na madeni juu.

Sent from my Redmi Note 3 using JamiiForums mobile app
Hapo mahali ni pagumu sana, pamenishughulikia kisawasawa, hadi sasa bado nina makovu. Kupaua is not a joke
 
sis
Finishing ni tamu kweli kweli, ila inatumbua pesa balaa, kupiga plaster, blandering ya kisasa na decoration zake kwenye ukuta wa tv, decoration za nje kwenye kona zote za nyumba na nguzo zake pamoja na Kufunga mkanda/kiuno na schemming Kwa ndani imetafuna 16m
sisi tusio mafundi haya maneno yanatutatiza sana.

1. Platers
2.blandering
3. Mkanda
4. Schemming

Mkuu tupe maarifa hapa ni vitu gani hivi?
 
Hapo mahali ni pagumu sana, pamenishughulikia kisawasawa, hadi sasa bado nina makovu. Kupaua is not a joke
Kupaua ilifika mahali nikamchukia fundi. Naona alidesign Paa la gharama wakati mimi ni kamandatu niliyechoka.
 
Back
Top Bottom