Mke mmeshashindwana kwa kila namna; kiuchumi hamuendi, kisocial hamuendi, kinidhamu n.k hamuendi, yaani ni tabu tupu na umeshafanya maamuzi kichwani ya kumrudisha kwao mara baada ya mavuno maana si kwa kutoelewana huku. Yaani katika wiki maelewano yanaweza kuwa ya siku mbili tu, siku zingine zote hata kusalimiana ni shida.
Katikati ya uelekeo wa kutekeleza maamuzi hayo, kuna kikwazo kikubwa; mtoto, binti mmoja mchangmfu anayeelekea kutimiza miaka mitatu hivi karibuni. Mtoto anakupenda nawe unampenda mno, kila muda wa kurudi kazini unapofika katoto kanasimama barazani kukulaki, yamekuwa mazoea ya kupendeza mno yanayokutia simanzi hata yakikosekana siku mbili tu. Vikelele vya kitoto ndani hadi anapolala nayo ni burudani nyingine.
Ukifikiria kuikosa burudani hii, pozi inagoma kuwekeka. Katika upendo huu wa kina, linakuja suala la kufikiria (imagination) ni namna gani binti huyu ataishi huko aendako kwa baba mlezi (lazima atapatikana tu).
Mbinu gani wadau ya kutumia kuneutralize hisia hasi hii?
Karibuni!