Unapenda mahusiano yako yadumu?

sabuwanka

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
691
Reaction score
757
Wapendwa wangu wana jukawaa salaam.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la mahusiano ya kimapenzi na ndoa kuvunjika hasa kwetu vijana, kugombana, kutofautiana, kupishana maneno ni jambo la kawaida kwasababu tunaingia katika mahusiano tukiwa na tabia tofauti tofauti na tena tumelelewa na kukulia katika mazingira tofauti.

Napenda nishauri kuwa inapotekea migogoro KUWA TAYARI KUJISHUSHA! Unyenyekevu wa mume kwa mwanamke unaokoa mahusiano, na unyenyekevu wa mke kwa mume huyeyusha hasira , kwa ustawi wa ndoa na mahusiano tuwe tayari kunyenyekeana, kuomba radhi , na kuzizungumzia tofauti zetu kwa upendo.

Ngumi, vibao, fimbo, havijengi wala kuimarisha mahusiano isipokuwa zinafanya kila asiyeridhika kuwa mguu upande!

Mwisho kanuni hiyo inatumika katika migogoro mingi isipokuwa ile ya uchepukaji hasa mwanamke kuchepuka

Tuendelee kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni
 
Ukiendekeza kujishusha kwa mwanamke utashtukia siku anakuingiza kidole kwenye njia ya haja kubwa..
 
Aki dunia ina mengi,

Piga picha mizimu ya nyumbani kwenu inakukwamisha usipate fedha na kufanikiwa vizur kimaisha, kisa umekataa mikoba ya babu.
Unapata mshahara lakin, hautosh mahitaji hasa kwa kujawa na mikasa ya kutumia pesa sana pindi ikipatikana tu.


Mke wako biashara zake zikikwama, kisa jambo hilo na ulimpa mtaji wa mamilioni si utaishi kumtukana kila siku pasipo hatia.

HAKIKA YESU NI KILA KITU.
 
Watu wanadai ndoa zenye mwaka mmoja, miwili mitatu zinavunjika....ni wapi huko mbona huku mtaani kwangu hazipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amina
 
Pia kua mwaminifu, mkweli, mjali mwenzio na jali hisia zake hata kama ni kidogo kiasi gani.

Nimepoteza wanawake wazuri kwa sababu za kijinga sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…