Unapigania Haki za Wanawake huku ukiwakatia Maji na Umeme

Unapigania Haki za Wanawake huku ukiwakatia Maji na Umeme

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Hakuna watu wanaoteseka na ukosefu wa maji na umeme kama Wanawake, wao ndio wanaohangaika visimani na ndoo kutwa nzima kutafuta maji kwa sababu wewe unayesimama jukwaani na kusema unawapigania umewakatia maji, sielewi hapa ni haki ipi hiyo ya Mwanamke unayoipigania ? Hivi haya mambo huwa mnayaelewa lkn au mnakarilishwa tu?

Raisi wa nchi masikini unakwenda kuji- commit na mambo ya global warming wewe ndiyo kinara na kuanza kutesa Wanawake na watoto ambapo si ajabu hata wewe ni mama wakati walioharibu Dunia hawafuati hayo masharti, huko Glasgow China hakwenda, Urusi hakwenda wala India unajua ni kwa nini?
 
Maajabu ya Mussa.

Jiwe alijua kilichomhusu, alichokuwa na ubavu nacho, asichokiweza akakifumbia macho nk. Ndiyo maana akaona yeye alikuwa wa maombi na nyungu zaidi si zaidi ya hapo!

Bwana Jumbe Brown mama anataka kuacha kuchimba gesi, mafuta na makaa ya mawe kama EU na Marekani kwa sababu ya tabia nchi?

Hiiiiii bagosha!

Wakati huo huo Japan, India, China nk wameuchuna?

Kwani kuchanganyikiwa ni nini basi?

Si walisema - tusiige ku*ya ya tembo?
 
Tumekuwa mahodari kueneza uzushi na chuki dhidi ya wengine.

Ya kwamba serikali ya awamu ya 5 ikaliona tatizo la umeme na kuamua kuwekeza TRILIONI 6.5 pale Mwalimu Nyerere ili ipatikane megawati 2215 hili nalo baya?

Awamu ya 6 Inaendeleza miradi ya maji chini ya Aweso.....hili nalo baya?

Awamu ya 6 ni mwendelezo wa awamu ya 5....unataka wakosoe baadhi ya hatua za serikali iliyopita ili kupatikane kitu gani?

Mathalani wako wanaokiri UMEME ulikuwa unakatika hata awamu ya 5.

Waziri wa nishati amesema kuwa Kati ya changamoto tulizonazo pia ni kufanyiwa SERVICE baadhi ya mitambo. je tuiache mitambo hiyo bila ya SERVICE?

Wote ni mashuhuda wa UKAME kuna anayebisha kuwa kina cha maji Mtera ,Kihansi na Pangani hakijapungua?

Sababu hizihizi za UKAME ndizo zilizopiga awamu ya 4 kutaka umeme wa GESI....na ndizo pia zilizopekea awamu ya 5 kutaka ujenzi wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE.

Mwisho wa siku ni ukosoaji tu usioangalia UHALISIA na kwa kuwa KIONGOZI ni jalala kama alivyokuwa hayati JPM basi KAZI IENDELEE TU. KAZI IENDELEE TU hakuna namna.

SIEMPRE JMT
KAZI IENDELEE
 
Leo Tena sikukuu imeshaanza lakini hakuna maji Wala umeme. Hivi Tanesco na Dawasco mnatuonaje?
Halafu tunaambiwa kazi iendelee. Kazi ipi vitu basic kabisa hatuvipati?
 
Back
Top Bottom