Unapokaribia kupata baraka za Mungu huwa kuna vikwazo, kwanini, majibu yapo hapa...

Unapokaribia kupata baraka za Mungu huwa kuna vikwazo, kwanini, majibu yapo hapa...

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
997
Unapokaribia mlango wa baraka kufunguliwa vikwazo utokea kwa nini

Danieli 10:13

Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

Katika kifungo hiki danieli alikuwa kafungu na kuomba ndani ya wiki 3,

Mungu alisikia maombi ya daniel siku ya kwanza na alituma malaika kuenda kumpa majibu lakini kutokana na vitu vya kiroho(vikwazo) daniel akaja kupata majibu siku ya 21.

Hivyo muda mwengine vikwazo utokea kipindi baraka zinakaribia ni adui kujaribu kuchelewesha baraka za Mungu.

Mungu anapo taka kufungua baraka katika maisha yako unapata vikwazo kama vile unakuwa na mawazo, kuchanganyikiwa, huzuni sababu ni adui anataka kuzuia baraka za Mungu.

Adui anapo ona kuna baraka katika Mbingu inataka kukufikia basi analeta mawazo, kuchanganyikiwa, huzuni ili kuchelewesha baraka kutoka kwa Mungu.

Hii ni kama Daniel, mbingu zilisikia maombi yake sababu adui anajua kuna baraka inaenda kwa daniel basi ikapelekea daniel kuchelewa kupata kutokana vita vya kiroho

Wakati mwengine ukiona vikwazo vingi kama huzuni, mawazo jua mlango wa baraka upo karibu inaweza kuwa baraka za kifedha au kuenda hatua nyengine ya kiroho,

Hivyo kama wewe ni mtu ulichaguliwa na Mungu upo katika hali hii jua kuna baraka mbele yako inakuja.

Lakini muda mwengine sio adui ni wewe mwenyewe unataka kupata vitu kwa nguvu sana kulingana na matamanio yako.

Ukiona upo kwenye hali ya kutaka kitu sana mara nyingi hupati mpaka pale utakapo achilia kuhitaji hicho kitu,

Unapo achilia tu kutohitaji hicho kitu uwa kinakuja kwa urahisi sana

Hii ni story yangu, "kuna kipindi nipo chuo nilipanga chumba sehemu, nikataka kuhama eneo hilo basi nilianza kutafuta chumba maeneo mengine,

Nilizunguka sana lakini sikufanikiwa kupata chumba nilichokuwa naitaji mwisho nikachilia(surrender) au kukubaliana na hali

Kesho yake nikapigiwa simu kama miujiza na rafiki mmoja akasema meshack kuna chumba huku ni kizuri,

Nilienda na kukuta chumba ni kizuri na mazingira ya nyumba yalikuwa mazuri".

Hii inafundisha muda mwengine ili miujiza itokee kwenye maisha yako ni pale unapo achilia(surrender) au kukubaliana na matokeo ,

Nilishindwa kwa nguvu zangu na hapo ndipo Mungu alianzia nguvu zake, nilipata chumba kama miujiza, Hivyo Mungu uwa anaanzia pale nguvu zako zinapoishia.
 
Back
Top Bottom