Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ikiwa Leo ni siku ya wanawake duniani ningependa nichangie mawili matatu.
Wanawake kama walivyo wanaume nao huwa Wana hisia za furaha na huzuni pia, kutofautiana katika ndoa ni Jambo la kawaida Sana kwasababu binadamu hatuja kamilika hivyo huwa tuna fanya makosa ima Kwa kujua au kutokujua au Kwa makusudi na wakati mwingine huwa hatukusudii Ila ndio udhaifu wetu kama wanadamu.
Sasa endapo imetokea tumewaudhi wenza wetu basi Busara inataka tuwaombe msamaha kwani huo ndio ubinadamu wetu, na Kwa kawaida binadamu yoyote angependa aombwe msamaha mara pale anapokosewa.
Sasa Kwa bahati mbaya Sana Sisi wanaume huwa tuna mtazamo mbaya kuhusu kuomba msamaha Kwa wenza wetu, tuna mtazamo kwamba kumwomba msamaha mwanamke ni kujishusha na kupunguza thamani yetu kitu ambacho si kweli, ukweli ni kwamba kuomba msamaha ni kuonyesha ukomavu na kuwajibika Kwa Yale makosa tuliofanya na hii itazidi kupandisha heshima yako mbele ya mwenza wako na kuonyesha kwamba unajali hisia zake na hivyo kumfanya akusamehe na akupende zaidi.
Hakuna Jambo linalo udhi kama umemkosea mwenza wako halafu badala ya Kumuomba msamaha badala yake unamwambia unampenda! Swali linakuja kichwani kama unanipenda kwanini umenikosea au kwanini umeniudhi?
Kwahiyo namna pekee ya kuweka mambo Sawa ni kuonyesha kwamba unajuta Kwa kile ulichofanya na unaomba radhi Kwa Hilo Kwa Nia Safi kabisa,na kufanya hivyo wala hakuta ondoa uanaume wako au kushusha thamani yako Bali utabakia kuwa mwanaume kamili na hadhi yako siku zote itabakia pale pale.
Kumbuka mapenzi ya kweli huwa haya angalii hadhi ya mtu Bali huangalia zaidi Utu WA mtu.
Katika siku hii ya wanawake duniani ningependa kutoa much love humu Jf Kwa Kalpana,Depal,To yeye, mademo iselle,baby zu Kwa kuwataja wachache.
Ni hayo Tu!