Unapomkosea mwanamke, Usimwambie Unampenda, badala yake muombe Msamaha!

Unapomkosea mwanamke, Usimwambie Unampenda, badala yake muombe Msamaha!

Hii migube gube ya dunia ya leo msamaha pekee wanaojua ni pesa.

Hata akukute upo uchi na demu mwingine ukituma muamala tu yameisha.
Yenyewe yanawaza upatu na VICOBA tu.
 
Ikiwa Leo ni siku ya wanawake duniani ningependa nichangie mawili matatu.

Wanawake kama walivyo wanaume nao huwa Wana hisia za furaha na huzuni pia, kutofautiana katika ndoa ni Jambo la kawaida Sana kwasababu binadamu hatuja kamilika hivyo huwa tuna fanya makosa ima Kwa kujua au kutokujua au Kwa makusudi na wakati mwingine huwa hatukusudii Ila ndio udhaifu wetu kama wanadamu.

Sasa endapo imetokea tumewaudhi wenza wetu basi Busara inataka tuwaombe msamaha kwani huo ndio ubinadamu wetu, na Kwa kawaida binadamu yoyote angependa aombwe msamaha mara pale anapokosewa.

Sasa Kwa bahati mbaya Sana Sisi wanaume huwa tuna mtazamo mbaya kuhusu kuomba msamaha Kwa wenza wetu, tuna mtazamo kwamba kumwomba msamaha mwanamke ni kujishusha na kupunguza thamani yetu kitu ambacho si kweli, ukweli ni kwamba kuomba msamaha ni kuonyesha ukomavu na kuwajibika Kwa Yale makosa tuliofanya na hii itazidi kupandisha heshima yako mbele ya mwenza wako na kuonyesha kwamba unajali hisia zake na hivyo kumfanya akusamehe na akupende zaidi.

Hakuna Jambo linalo udhi kama umemkosea mwenza wako halafu badala ya Kumuomba msamaha badala yake unamwambia unampenda! Swali linakuja kichwani kama unanipenda kwanini umenikosea au kwanini umeniudhi?

Kwahiyo namna pekee ya kuweka mambo Sawa ni kuonyesha kwamba unajuta Kwa kile ulichofanya na unaomba radhi Kwa Hilo Kwa Nia Safi kabisa,na kufanya hivyo wala hakuta ondoa uanaume wako au kushusha thamani yako Bali utabakia kuwa mwanaume kamili na hadhi yako siku zote itabakia pale pale.

Kumbuka mapenzi ya kweli huwa haya angalii hadhi ya mtu Bali huangalia zaidi Utu WA mtu.

Katika siku hii ya wanawake duniani ningependa kutoa much love humu Jf Kwa Kalpana,Depal,To yeye, mademo iselle,baby zu Kwa kuwataja wachache.

Ni hayo Tu!
Usikubali makosa
 
Hawa watu wa Jamii ya JF ni watu wa wapi? Yani umkosee mwanamke halafu usiombe msamaha 🤣🤣 kweli watu wanaishi katika ndoto.

Scenario 1: Mwanamke akukute kwa macho yake unamsaliti. Kisha ukatae katu katu kuwa hujamsaliti

Baada ya hapo aku accuse unamsaliti then unakataa kata kata kuwa sijakusaliti. Kisha mwanamke anasahau ulimsaliti na kukupa mapenzi mengiiiii kwa sababu tu umekataa kukubali kuwa wewe ni msaliti🤣🤣🤣

Najiulza hao ni wanawake wa wapi? Wa JF?

Wahenga walisema 'akili si nywele'. Akasikika mwana JF mmoja 'mwalimu na vuzi Je?'
Chief

Lunch ya Leo IPO juu yangu

Waambie ETUGRUL BEY atasimamia show nzima
 
Hapo ndo mnapokosea
Unaweza ukawa umepata wife material,anaejielewa na kujua wajibu wake kwa mumewe ila sasa hii attitude yako ikampoteza!
Unapaswa umsome mwanamke ulie nae ni wa aina gani usiishi kwa kukariri!
💪💪💪
 
Ni kweli umeongea point muhimu Sana

Hapa nimezungumzia makosa mbali mbali ambayo kama wanadamu huwa inatokea tutakoseana Kwa namna moja au nyingine.

Lakini point yako inategemea na mazingira vile vile, je kama umekamatwa live katika eneo la tukio na ushahidi uko wazi hapo bilashaka kukiri ukweli na kuomba msamaha hakukwepeki.
Hata ukamatwe on spot mwanaume unapaswa kukataa kwamba sio ww.

Mwanamke : baba flani nilikua naambiwa tu na watu leo kwa macho yangu nakushuhudia upuuzi unaofanya, hv kweli we wa kunisaliti na huyu Malaya?

Mwanaume: hapana mama flani utakua umenifananisha sio mm. Mi sijawahi kukusaliti
 
Hata ukamatwe on spot mwanaume unapaswa kukataa kwamba sio ww.

Mwanamke : baba flani nilikua naambiwa tu na watu leo kwa macho yangu nakushuhudia upuuzi unaofanya, hv kweli we wa kunisaliti na huyu Malaya?

Mwanaume: hapana mama flani utakua umenifananisha sio mm. Mi sijawahi kukusaliti
Chief

🤣🤣 Umenikumbusha Ile nyimbo ya sheggy he wasn't me!

Ila mambo mengine ni rahisi kusema kuliko hali halisi ilivyo
 
Kosa kubwa sana mwanaume
kutamka "nisamehe" kwa mwanamke.
Ambae si mama ako na mko kwny mahusiano

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Chief

Naomba tukubaliane kutokukubaliana juu ya jambo hili

Wewe endelea kuwa na mtazamo juu ya Hilo nami niwe na mtazamo kwamba wanawake wanastahili kuombwa msamaha
 
Back
Top Bottom