Unapopata mtoto katika umri wa miaka 70 uhakika wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 20 au 30 ni mdogo

Unapopata mtoto katika umri wa miaka 70 uhakika wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 20 au 30 ni mdogo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Unapopata mtoto ukiwa na umri mkubwa, kikubwa unachoweza kumpa ni busara ulizozikusanya kwa miaka mingi. Uwezekano wa kusherehekea mahafali yake ya elimu ya juu ni mdogo sana.

1674014347456.png

David Foster mwenye umri wa miaka 73 akiwa na mke wake wa ndoa ya tatu na mtoto wao.

Watoto wa uzeeni wana muda mwingi wa kucheza na wazazi wao kwani huwa wamesha staafu. Kwa wale walio pangilia maisha na wana vitega uchumi, uzeeni pesa inakuwepo.

Watoto wa ujanani wanazaliwa wazazi wakiwa katika harakati za kupambana na maisha. Wengine wazazi bado ni wanafunzi, wazazi wengine wanafanya kazi masaa 12 nyumbani wanaingia kulala tu.

Uamuzi ni wako kuzaa ujanani au uzeeni.
 
Unapopata mtoto ukiwa na umri mkubwa, kikubwa unawchoweza kumpa ni busara ulizozikusanya kwa miaka mingi. Uwezekano wa kusherehekea mahafali yake ya elimu ya juu ni mdogo sana...
Ingawa maisha ni magumu sana kwa ujumla wake, lakini kuwa na mtoto mapema katika ujana naona ni bora mara elfu kuliko uzeeni.

Jamii kwa ujumla, nature kwa ujumla na hata Mungu kwa ujumla ndivyo inavyotaka viumbe wafanye.

Nje ya mada Sky Eclat ni kama ulipotea hivi kwa muda hatujakuona hapa, nafurahi sana kukuona.
 
Unapopata mtoto ukiwa na umri mkubwa, kikubwa unawchoweza kumpa ni busara ulizozikusanya kwa miaka mingi. Uwezekano wa kusherehekea mahafali yake ya elimu ya juu ni mdogo sana...
Yani ushawapangia watu kuzaa tayari, ila wazae ujanani au uzeeni?

Hujui kuna watu hawataki kuzaa kabisa?
 
Unapopata mtoto ukiwa na umri mkubwa, kikubwa unawchoweza kumpa ni busara ulizozikusanya kwa miaka mingi. Uwezekano wa kusherehekea mahafali yake ya elimu ya juu ni mdogo sana...
Cha Msingi ni kwamba umempata mtoto na umemuona

Kuna vijana wadogo sana waliacha wake zao wakiwa na mimba

Urijali huo
 
Ingawa maisha ni magumu sana kwa ujumla wake, lakini kuwa na mtoto mapema katika ujana naona ni bora mara elfu kuliko uzeeni.

Jamii kwa ujumla, nature kwa ujumla na hata Mungu kwa ujumla ndivyo inavyotaka viumbe wafanye.

Nje ya mada Sky Eclat ni kama ulipotea hivi kwa muda hatujakuona hapa, nafurahi sana kukuona.
Upo sahihi kbsa mkuu
 
Kwa maisha ya Africa kuzaa mtoto ukiwa beyond 50 years Ni sawa sawa na kujitakia kifo Cha mapema..

Wenzetu wazungu wametuzidi kete nyingi Sana katika kujipanga kimaisha.
 
Back
Top Bottom