Unapopatwa na huzuni, hasira, msongo wa mawazo AU maumivu ya moyo... Tulizo lako ni nini?

Unapopatwa na huzuni, hasira, msongo wa mawazo AU maumivu ya moyo... Tulizo lako ni nini?

Kila mmoja wetu hupitia nyakati ngumu. Wapo wanaopoteza wapendwa wao, hukatishwa tamaa, husalitiwa, hukosa kazi, hupitia matatizo ya kifamilia au ya kifedha. Wakati huo, kila mtu hutafuta njia yake ya kupata utulivu.

Wengine husali na kumtegemea Mungu. Wengine husoma vitabu, husikiliza muziki, hufanya mazoezi, huongea na marafiki, hutembea peke yao, hulia ili kupunguza maumivu, au hujishughulisha na kazi.
Lakini pia wapo ambao, kutokana na maumivu, hujikuta wakikimbilia pombe, sigara, dawa za kulevya au tabia nyingine ambazo baadaye huongeza matatizo badala ya kuyapunguza.

Hakuna maisha yasiyo na changamoto. Swali ni, wewe unapokumbana na huzuni, hasira, msongo wa mawazo au maumivu ya moyo, ni kitu gani hukupa utulivu na kukusaidia kusonga mbele?
Nakula weed then naenda kuoga nalala, nikiamka nakuwa mpya kabisa.
 
Kila huzuni ina sababu, huwezi kutikiswa na kitu kisichokuhusu

Kila kikundi cha watu duniani kina madaraja.. Namaanisha

1.hadhi ya juu

2.ya kati

3.ya chini

Ni kanuni huamua madaraja na si watu wenyewe

Kwa hali ilivyo dunia sasa mbali na hata sisi Tz.!

Ni mchapuo wa wa Tabaka la juu kujishusha kwenye uongozi kupisha asili ichukue nafasi

Kuruhusu Ndezi wachache wa tabaka la kati na wale wa chini to lead

Na gharama yake ni matumizi ya uraibu wa kujifariji kutengeneza mbingu kuzimu

Naamisha nini.?

Usishangae Teja vituoni ukambeza ni Chifu wa kijijini kwenu aliyekosa matumaini
 
ni kitu gani hukupa utulivu na kukusaidia kusonga mbele?
Maji ya kunywa
Kitu chochote cha kutafuna especially chenye sukari kidogo km bites
Sehemu tulivu isiyo na kelele
Sehemu yenye moto unaofuka moshi niote moto hapo km gari limewaka basi washa jenereta
Sehemu ninayoweza kwenda kumgonga mtu na kumkojolea

Hivyo vitu vinanipa utulivu
 
Watoto.. haswa ile stage anajifunza kuongea anaboronga maneno, Mungu anijalie nipate 7 au 8 au zaidi.. hawajali una pesa, una stress, una chumba kimoja au bangaloo, unapitia nini yeye anataka attention Yako tu.

Raha sana kuitwa baba na mtoto haswa kama mnafanana
 
Kila mmoja wetu hupitia nyakati ngumu. Wapo wanaopoteza wapendwa wao, hukatishwa tamaa, husalitiwa, hukosa kazi, hupitia matatizo ya kifamilia au ya kifedha. Wakati huo, kila mtu hutafuta njia yake ya kupata utulivu.

Wengine husali na kumtegemea Mungu. Wengine husoma vitabu, husikiliza muziki, hufanya mazoezi, huongea na marafiki, hutembea peke yao, hulia ili kupunguza maumivu, au hujishughulisha na kazi.
Lakini pia wapo ambao, kutokana na maumivu, hujikuta wakikimbilia pombe, sigara, dawa za kulevya au tabia nyingine ambazo baadaye huongeza matatizo badala ya kuyapunguza.

Hakuna maisha yasiyo na changamoto. Swali ni, wewe unapokumbana na huzuni, hasira, msongo wa mawazo au maumivu ya moyo, ni kitu gani hukupa utulivu na kukusaidia kusonga mbele?
 

Attachments

  • hang.png
    hang.png
    131.7 KB · Views: 10
Back
Top Bottom