Unapoteza vyote...

Daah Uzi huu umeniuma sana

KUNA JAMAA NILIMUAZIMA SH ELFU 25 yangu ili atoe hela ya kufanyia sherehe ya kumaliza form four ashone na sare, tangu amalize shule mpaka leo hajibu meseji zangu.

Maadamu napafahamu kwao. Siku zikinipanda namzukia

Sitaki utani kwenye pesa zangu.!!!
 

Pole
 
Nilikomaa na madam mmoja mambo ya kuazima hela halafu anajifanya kama kupotezea weeeeeeee mbona alitoa hela yangu japo kwa mafungu mafungu na ukaribu wetu ukaishia hadi leo
 
Nilikomaa na madam mmoja mambo ya kuazima hela halafu anajifanya kama kupotezea weeeeeeee mbona alitoa hela yangu japo kwa mafungu mafungu na ukaribu wetu ukaishia hadi leo

Hahahaaaa!

Ilibidi uwe mkali eeh?
 
Halafu, hebu tuache kujifanya wote ni wema sana humu.

Nina imani hata wazikaji wapo pia.

Tupate basi na ushuhuda wa ulivyomzika mshikaji wako hela zake.

Hahahaaaaa..lets keep it 100 folks.
 
Duuh... pole sana dada Raynavero kwa kupoteza rafiki.

mimi ilikuwa ni 15k tangu mwaka 2014 hadi leo mwanangu Paschal hataki kabisa kupokea simu yangu hata kama namtafuta kwa mambo mengine.
Ahsante yaani wanadamu bwana kwenye pesa daah!tunabadilika sana! Tuko tayari kupoteza watu wetu!pesa inafanya utu uishe!
 
Nshapoteza wengi tu wa kike na kiume.
 
Kwa rafiki siwezi kopa pesa nyingi, ambazo nitashindwa rudisha, na Mara nyingi huwa tunasaidiana ndio misingi ya urafiki wetu. Nachukia kukopa.
 
Jamaa angu kodi iliisha kabla boom halijatoka na akiba aliyokua nayo ni kodi ya mwezi mmoja tuu (tsh 30,000/=). Akaniomba nimkopeshe nyingine ya miezi miwili atanilipa Mzigo ukitema.

Tangu nimkopeshe hiyo hela ashapokea boom mara mbili, kapokea hela ya field lakini bado hajawah kunirudishia! Na bahat mbaya mim huwaga sina ujasiri wa kumdai mtu, hasa rafiki angu hivyo nikawa nasubiri tuu anifnyie kama 'hisani'. Jamaa hajawah kukumbuka deni, na yeye ndiye anaeua urafiki, zile sim za mara kwa mara zilianza kupungua mwishowe zikaisha kabisa..
 
nimepoteza marafiki wa tatu na ex girlfriend mmoja na pesa pia zimeenda nao....

hawa marafiki haina shida ila huyu ex popote ntakapokutana naye ntamzingua maana hela yenyewe aliyochukua nilisikia aliendaga kumlipia ada bwana ake mpya yani ndio hasira zinazid mamaeee
 
dah mi kuna mtu nilimpa laki sita baada ya kumdai sana akawa ananilipa elfu 50 mara elfu 30 dah hahahaaaaaaaa
 
Aisee mimi kuna dem aliniomba nimuazime elf10 atanirudishia sikumuuliza utairejesha lini na nilitaka nimsaidie tu ila nilikausha kwanza ili nimpime imani imepita kama mwezi harudishi akanitumia sms atairejesha baada ya week2 napo mwezi ukakata tena hola kumbuka alikua rafiki na story za Hapa na pale kwa sana tu ila akanipotezea mazima na mm nilitaka kumpima imani tu
 
rafiki wa kweli hamuwezi kuuwa urafiki sababu ya deni,mnazinguana tu kidogo yanaisha maisha yanaendelea.Mimi rafiki akimeza hela yangu wala sigombani naye,tena namuombea kwa mungu apate,siku akishakuwa na hela na akijasahau kama alitafuna hela yangu na mie natafuna pesa yake au mali yake tena yenye thamani zaidi ya kile alichochukuwa kwangu,akija juu namkumbusha.maisha yanaenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…