Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mwamba alienda dukani kununua kitu akarudishiwa chenji. Sasa kwa vile jamaa alikuwa na stress kwa haraka haraka akajua mwenye duka kamzidishia chenji, hivyo akarudisha hela nusu kwa mwenye duka akimwambia kuwa amemzidishia. Mwenye duka nae hakukataa akapokea chap chap na kuzirudisha ndani ya droo la hela.Katika mihangaiko ya hapa na pale unaweza kwenda dukani ama sokoni inapotokea muuzaji kakuzidishia 'chenji" unachukua hatua gani!??
Binafsi huwa narudisha
Wewe je? Wafanyabiashara wanapitia changamoto sana
Ilikuaje hiyo mkuu 😂😂narudisha na imewahi nisaidia kumpata binti mmoja hivi muuza duka
tenda wema uende zako mkuu, usitegemee malipoIlikuaje hiyo mkuu 😂😂
😂Hio tunaita muosha kaoshwaMwaka 2009 nilitumwa umeme Wa LUKU kipindi hiki umeme ulikuwa unanunuliwa Tanesco tu
Baada ya kupewa elfu tano nikatoa buku kwa ajili ya kununulia Peni na rula sikumuambia MTU .
So ile elfu nne nikaenda nayo kununua umeme
Kufika pale Tanesco yule jamaa aliniwekea umeme wa laki nne
Sasa umeme ulipomaliza muda mrefu bila kukatika watu hawakua wanajua .
Then mwenye nyumba akawa anachukua hela za umeme Kama kawaida huku umeme ukiendelea kuwepo
Kimbembe umeme ulipoisha Tanesco walianza kukata hela yao kila tukinunua .
Ni mambo kama haya haya yanatokea madukani na kwa mawakala lakini chuma ulete ndo wanalaumiwa.Asubuhi moja nimewahi CRDB bank ku deposit kama 2m plus. Nikajaza ile slip nikamaliza nikampa teller halafu nikatoa hela nikaziweka juu pale sijamuingizia kwenye kidirisha chake. Teller yuko busy anaingiza muamala. Kamaliza kanipa slip yangu, nikabaki namwangalia na yeye ananiangalia kama ananiuliza unasubiri nini hajui kama sijampa hela. Nikamwambia naomba nikuzawadie hizi hela, alishtuka sana akaziwahi chap akahesabu zimetimia akanishukuru huku akisema ameamka na stress sana hio siku,akasema ningeondoka angehangaika mwisho wa siku bila kujua short imetokea wapi.
Mwenye nyumba alitoa maelezo gani baada ya nyinyi kushangaa makato? Ila muuza LUKU mwezi huo alikula bonge ya hasara.Kimbembe umeme ulipoisha Tanesco walianza kukata hela yao kila tukinunua .
Kamserereko ...Unapozidishiwa chenji huwa unarudisha?