Kuna mwamba alienda dukani kununua kitu akarudishiwa chenji. Sasa kwa vile jamaa alikuwa na stress kwa haraka haraka akajua mwenye duka kamzidishia chenji, hivyo akarudisha hela nusu kwa mwenye duka akimwambia kuwa amemzidishia. Mwenye duka nae hakukataa akapokea chap chap na kuzirudisha ndani ya droo la hela.
Mwamba ameenda kufika mbele ndo akili zinamrudia kuwa hela aliyokuwa nayo ni nusu. So ikabidi arudi kwa mwenye duka ili amrudishie zile hela alizodai kuwa kamzidishia. Cha ajabu alivyofika kule mwenye duka kagoma kumpa zile hela, eti chenji aliyomrudishia ilikuwa ni sawa. Jamaa kwa hasira kaondoka huku akimtukana muuza duka kuwa mzulumati. Sasa hapo nani anastahili lawama? Jamaa wema umemponza.