Unapozidishiwa chenji huwa unarudisha au ndio wimbo wa Albert Mangwear "kimya kimya" mwendo wa haraka mbele

Unapozidishiwa chenji huwa unarudisha au ndio wimbo wa Albert Mangwear "kimya kimya" mwendo wa haraka mbele

Katika mihangaiko ya hapa na pale unaweza kwenda dukani ama sokoni inapotokea muuzaji kakuzidishia 'chenji" unachukua hatua gani!??

Binafsi huwa narudisha
Wewe je? Wafanyabiashara wanapitia changamoto sana
Narudisha
 
Kwa wengine woooote narudisha chenchi,

Ila sio kwa Konda wala Poti

Tena hasa trafiki wale jamaa hata ningekuwa na biashara akiuliza naongeza bei *****, wana roho chafu sana
 
Mwenye nyumba alitoa maelezo gani baada ya nyinyi kushangaa makato? Ila muuza LUKU mwezi huo alikula bonge ya hasara.
Hakuna maelezo aliyowapa maana alikuwa ni mzazi wangu

Na hela zilikuwa zinapitia kwake hakuna kuuliza maswali.

Sema baada ya kukua na kujitambua niliwashauri wapangaji wale waliokuwa wanafanya biashara.

Wafunge mita yao wenyewe kutoka tanesco la sivyo wataumia

So walifanya hivyo maana wapangaji ni watu wa frame.
 
Uaminifu ni mtaji japo Kuna mzungu aliwai SEMA you will die poorly Aki remarks mama mmoja baada ya kumrudishia wallet yake aliyo idondosha 😊😊😊
Katika mihangaiko ya hapa na pale unaweza kwenda dukani ama sokoni inapotokea muuzaji kakuzidishia 'chenji" unachukua hatua gani!??

Binafsi huwa narudisha
Wewe je? Wafanyabiashara wanapitia changamoto sana
 
Mpaka konda nimeshawahi kumrudishia.
Kuna kisa kimoja nikishawahi kusema hapa.

Kuna teacher tunajuana aliazima laini yangu ya voda na modem ili atumie.
Kwa kuwa laini haikuwa na salio nikamwambia akaweka MPESA.

Nikaona anarudi ana uso fulani hivi akasema hebu braza tuongee pembeni kwanza, nikasema nini! Akasema dogo kuzidisha pesa kaweka 20,000 badala ya 2,000 kwa hiyo tugawane. Nikasema sio vizuri kwa sababu dogo mwenyewe ni mwajiriwa tu pale itakuwa hasara kwake.

Teacher akamaindi akasema shauri yako, tutakufa masikini.
 
Kuna mwamba alienda dukani kununua kitu akarudishiwa chenji. Sasa kwa vile jamaa alikuwa na stress kwa haraka haraka akajua mwenye duka kamzidishia chenji, hivyo akarudisha hela nusu kwa mwenye duka akimwambia kuwa amemzidishia. Mwenye duka nae hakukataa akapokea chap chap na kuzirudisha ndani ya droo la hela.

Mwamba ameenda kufika mbele ndo akili zinamrudia kuwa hela aliyokuwa nayo ni nusu. So ikabidi arudi kwa mwenye duka ili amrudishie zile hela alizodai kuwa kamzidishia. Cha ajabu alivyofika kule mwenye duka kagoma kumpa zile hela, eti chenji aliyomrudishia ilikuwa ni sawa. Jamaa kwa hasira kaondoka huku akimtukana muuza duka kuwa mzulumati. Sasa hapo nani anastahili lawama? Jamaa wema umemponza.
Mwenye duka ndiye mwenyekosa kwasababu. Anaufahamu ukweli
 
Unaweza chukua kumb
Ndio maisha Hayo mm sirudishagi Kuna siku nilienda kwa wakala kueka buk mbili nibetie maana bum lilikua limeisha akaweka buk 20 Sasa scenario hiyo unarudishaje hela ....take it ukifika muda wa kurudisha utarudisha tu

Uaminifu ni mtaji japo Kuna mzungu aliwai SEMA you will die poorly Aki remarks mama mmoja baada ya kumrudishia wallet yake aliyo idondosha 😊😊😊
Sasa Mkuu niambiye mtu amekuzidishia elfu kumi unapeleka wapy hiyo au kama ni zaidi kumbuka sadaka s lazima ukatoe kanisani/masjid ata kurudisha ni fadhila
 
Mimi inategemea ni kiasi gani cha pesa na mfuko wangu umekaaje siku hiyo kwahiyo naweza au nisiweze kurudisha
 
Huwa narudisha na sio mara moja kuzidishiwa hela hii imekuwa kama kawaida hata nikisaulika na konda nitahakikisha hela yake anaipata na endapo gari lake litaondoka. Niheri nikawapa wale wanao omba msaada barabarani.

Tena baada ya kurudisha huwa napata amani ya pekee sana moyoni mwangu.
 
Katika mihangaiko ya hapa na pale unaweza kwenda dukani ama sokoni inapotokea muuzaji kakuzidishia 'chenji" unachukua hatua gani!??

Binafsi huwa narudisha
Wewe je? Wafanyabiashara wanapitia changamoto sana
Kuondoka na pesa isiyo yako huku ukijua ni dalili ya ufukara uliopiliza na kutostaarabika.
 
Up
Huwa narudisha na sio mara moja kuzidishiwa hela hii imekuwa kama kawaida hata nikisaulika na konda nitahakikisha hela yake anaipata na endapo gari lake litaondoka. Niheri nikawapa wale wanao omba msaada barabarani.

Tena baada ya kurudisha huwa napata amani ya pekee sana moyoni mwangu.
Upo kama mimi huwa nafurahia sana lakini ukitaka kusepa nayo Ile roho waga inaumia ndani kwa ndani najiuliza kama ndo biashara ingekuwa yangu
 
Up

Upo kama mimi huwa nafurahia sana lakini ukitaka kusepa nayo Ile roho waga inaumia ndani kwa ndani najiuliza kama ndo biashara ingekuwa yangu
Nilipokuwa sina utashi na uelewa wa kina wa mambo yaletayo faraja na utulivu ndani ya moyo niliweza kufanya hivo ila tangu nianze kutambua mambo kwa namna ambavyo yapo na yanatakiwa kuwa niliacha kabisa.

Mambo ya kukaa na maumivu ndani ya moyo wako kwa jambo linalowezekana nani anapenda
 
Sijawahi kuchukua hela ya kuzidishiwa, nakumbuka siku moja nilikuwa na shida sana ya hela, kwenda kwa wakala wa Airtel money badala ya 100k akanipa 110k, nikamrudishia 10k yake mimi nikaondoka zangu. Shida ni kwamba hata ukiichukua utailipa tu tena pale ambapo huwezi kutarajia.
 
Back
Top Bottom