Unaridhika na Mwenza uliyenaye au unavumilia tu?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,450
Reaction score
19,184
Wakati mwingine tunajidanganya kwa jina la 'uvumilivu' wakati ndani ya moyo tumechoka.


Kuridhika ni amani. Ni kula na kucheka na mtu kutoka moyoni na kulala bila mawazo.

..........Lakini kuvumilia... ni kuishi kwa matumaini ya kwamba 'siku moja atabadilika'.

Tusidanganyane. Sio kila uhusiano unaodumu una maana. Baadhi yetu tumebaki kwa sababu ya woga wa watu watasemaje kutokana na muda tulioupoteza.

Lakini kumbuka, maisha ni mafupi sana kuvumilia mtu asiyekuthamini.

Kuridhika kunaleta tabasamu halisi.

Ulipoamua kupenda, ulitaka amani sio vita ya kila siku. Chagua unachoweza kuishi nacho milele, sio unachoweza 'kustahimili' tu.

Furaha yako pia ina thamani."
 
Hakuna mwanadamu mkamilifu kila mmoja ana upungufu hapa ama pale. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta ambaye ana mapungufu ambayo unaweza kuhimili muanze maisha.

Kurafufa ambaye utaridhika kwa kila kitu basi ushike udongo uumbe wa kwako ila si mtoto aliyetoka kwenye tumbo la mwanamke.

Tukiacha maisha ya kufikirika na kuangalia uhalisia, hayo mambo ya kutaka uridhike kwa kila kitu hayatakuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…