Unaridhika na Mwenza uliyenaye au unavumilia tu?

Unaridhika na Mwenza uliyenaye au unavumilia tu?

Hakuna mwanadamu mkamilifu kila mmoja ana upungufu hapa ama pale. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta ambaye ana mapungufu ambayo unaweza kuhimili muanze maisha.

Kurafufa ambaye utaridhika kwa kila kitu basi ushike udongo uumbe wa kwako ila si mtoto aliyetoka kwenye tumbo la mwanamke.

Tukiacha maisha ya kufikirika na kuangalia uhalisia, hayo mambo ya kutaka uridhike kwa kila kitu hayatakuwepo
Asante sana Hassan
 
35 years na mke wangu, na alikuwa na tabia za hovyo mpaka tukatengana for 3 good years, sasa kila mmoja wetu kabadilika na kuwa sambamba na mwenzake.
Hongera sana, lakini tunarudi kule kule kwenye hoja yangu ya mwanzo, ukubwani mtu huwa anabadilika kwa ajili ya maslahi fulani, anaamua kujizuia tu na siyo kwamba anakuwa ameachana na tabia zake za hovyo.
 
Wakati mwingine tunajidanganya kwa jina la 'uvumilivu' wakati ndani ya moyo tumechoka.

Kuridhika ni amani. Ni kula na kucheka na mtu kutoka moyoni na kulala bila mawazo.

..........Lakini kuvumilia... ni kuishi kwa matumaini ya kwamba 'siku moja atabadilika'.

Tusidanganyane. Sio kila uhusiano unaodumu una maana. Baadhi yetu tumebaki kwa sababu ya woga wa watu watasemaje kutokana na muda tulioupoteza.

Lakini kumbuka, maisha ni mafupi sana kuvumilia mtu asiyekuthamini.

Kuridhika kunaleta tabasamu halisi.

Ulipoamua kupenda, ulitaka amani sio vita ya kila siku. Chagua unachoweza kuishi nacho milele, sio unachoweza 'kustahimili' tu.

Furaha yako pia ina thamani."
Ndugu mdau,
suala la ustahimilivu na subra ni la lazima kwenye mahusiano au ndoa yoyote ile. In fact hakunaga mahusiano yasiyo kua na changamoto ikiwa ni pamoja na kuchokana. Na dawa ya hilo ni ustahimilivu na subra.

Na kwa maoni yangu,
hali hiyo hua ni mapito muhimu zaidi sana katika kufanya mahusiano au ndoa kua imara zaidi, ya heshima zaidi, yenye furaha na amani zaidi kadiri siku zinavyosonga hususani baada ya kuvuka hali hiyo.

Mapenzi sio excitement za kila siku bali ni ule utofauti wa ladha za nyakati tofauti tofauti za shida na raha.

usikate tamaa,
usiogope wala kusita kuanzisha mahusiano mengine.
Daima nasisitiza kua, ni muhimu sana kubadili changamoto tunazokumbana nazo kua fursa muhimu sana ya kukufanya uwe makini zaidi na bora zaidi kuelekea katika mahusiano mengine 🐒
 
Asante sana kwa ushauri mzuri. 🙏
 
Back
Top Bottom