Ile methali ya mtaka cha uvunguni sharti ainame tumeisahau?
Na kuna wakati mchonga alituonya kuwa wale wanaosema kule nje kuna hela nyingi, siku mkiletewa hela ya wauza bangi mtafanyaje?
Kimsingi, maadili ya magharibi yamemomonyoka sana na washaamua kuleta hilo zahma dunia nzima.
Historia inaonesha shule nyingi hapa Tanganyika na wakati wa Deusche Ostafrika zilimilikiwa na mashirika na dini hasa Anglican, Lutheran na Catholics. Moja ya msingi wa Imani ni kutii amri 10 za Mungu na kufuata biblia kama msaafu kimaadili hasa kwenye kuzuia uzinzi na uasherati.
Baada ya Uhuru kupatikana, JKN na waliofuatia walibaki wakiamini sheria za kuzuia uasherati na wenye mimba walifurushwa shule.
Misaada imetufanya 'tuiname' na sasa kama wenye mimba wanaruhisiwa kusoma na ruksa kurejea baada ya kujifungua, msingi wake, sheria ya kuzuia uasherati mashuleni sioni kama inasimama tena.
Ngamia huanza kuongoza kwato, baadae miguu, baadae kichwa, baadae mwili mzima na kajumba huwa kanajiangukia.
Tukifanya tathmini, sijui ngamia Yuko stage gani kwenye kutaka kuzama ndani ya nyumba yetu.
Profesa Mkenda 'anakomaa' ila wale wanaotoa budget support wizara ya Elimu kama wataona anazuia 'koneksheni' je atabaki kazini?
Kama alivyowahi kugoma kusaini kutoa vibali vya sukari kinyume na utaratibu, je, wazeiya wakimwaga pichi na kushinikiza mitaala ipitiwe upya ili masuala ya 'upinde wa mvua' kuwa sehemu ya mafunzo, na sio lazima kuona kuna he na she ila tukaaminishwa wanadamu ni zaidi ya he na she, je, prof ataweza kusimama kama Qatar kuzuia mafuriko ya mmomonyoko wa maadili bila support ya toka juu.
Wakati huzungumza na kufichua mengi yaliyositirika.
Mchana mwema!