Unashauri 2025 Mbunge wa jimbo gani ajizuie kugombea tena kiti hicho kuepuka fedheha ya kushindwa?

Unashauri 2025 Mbunge wa jimbo gani ajizuie kugombea tena kiti hicho kuepuka fedheha ya kushindwa?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Japo wabunge wengi wametekeleza vizuri sana wajibu, kazi na majukumu yao hasa ya kitaifa kupitia bunge, kwa weledi na umahiri mkubwa, lakini kutokana na hali halisi huko majimboni kwao inaonekana hawatakua na nafasi nzuri na ya uhakika kuchaguliwa tena katika awamu nyingine kwenye uchaguzi ujao....

Hii ni kuanzia kwenye mchujo wa vyama. Na hii ni kutokana na sababu mbalimbali, mathalani kutokuonekana jimboni kwa kipindi kirefu, kutokuonekana katika vikao vya bunge kuishauri, kupendekeza jambo au kuikosoa serikali, kutokuchangia chochote kwa maandishi au kuzungumza bungeni kwa niaba ya wananchi wake, kutokuonekana katika shughuli za kijamii kama vile misiba, mahafali, sherehe, dua na maombi jimboni, kutokushiriki shughuli za maendeleo, kutokuhudhuria vikao baraza la madiwani, wala kuitisha mikutano ya hadhara jimboni, kuzungumza na wananchi kuhusu uelekeo wa maendeleo ya jimbo na sababu nyingine za kiutendaji sisizo za kibinafsi, na kwahivyo mbunge hoyo awe na hekima na utulivu, pension yake aitumie vizuri kujijenga kimaisha, kuliko kuwekeza kutetea kiti cha ubunge.

Ni vizuri kuzingatia kumshauri mbunge na mwanasiasa wa jimbo lako, itapendeza zaidi.

Ikiwa mwanasiasa huyo bado anafaa, usisite kumtia moyo na kumshauri maeneo ambayo, yafaa ayafanyie kazi zaidi na kwa nguvu zaidi :whatBlink:
 
Japo wabunge wengi wametekeleza vizuri sana wajibu, kazi na majukumu yao hasa ya kitaifa kupitia bunge, kwa weledi na umahiri mkubwa, lakini kutokana na hali halisi huko majimboni kwao inaonekana hawatakua na nafasi nzuri na ya uhakika kuchaguliwa tena katika awamu nyingine kwenye uchaguzi ujao....

Hii ni kuanzia kwenye mchujo wa vyama, kutokana na sababu mbalimbali, mathalani kutokuonekana jimboni kwa kipindi kirefu, kutokuonekana katika vikao vya bunge, kutokuchangia chochote kwa maandishi au kuzungumza bungeni, kutokuonekana katika shughuli za kijamii jimboni, kutokushiriki shughuli za maendeleo kuhudhuria wala kuitisha mikutano ya hadhara jimboni, kuzungumza na wananchi kuhusu uelekeo wa maendeleo ya jimbo na sababu nyingine za kiutendaji sisizo za kibinafsi, na kwahivyo awe na hekima na utulivu, pension yake aitumie vizuri kujijenga kimaisha, kuliko kuwekeza kutetea kiti cha ubunge.

ni vizuri kuzingatia kumshauri mbunge na mwanasiasa wa jimbo lako, itapendeza zaidi.

Ikiwa mwanasiasa huyo bado anafaa,
usisite kumtia moyo na kumshauri maeneo ambayo, yafaa ayafanyie kazi zaidi na kwa nguvu zaidi 🐒
Bishop Josephat Gwajima, kaa mbali na Kawe
 
CCM nzima

Happy new month ladies and gentlemen
Wote

Tuanze Upya 🐼
20240530_215249.jpg
 
Back
Top Bottom