Unashughulika vipi na watu wa aina hii....

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Hello JF...

Wewe ni mtu muhangaikaji kama wengine hapa mjini.
Mtu anakulilia shida hasa ni nduguzo. Unamsaidiaga mara kwa mara pale unapokuwa nacho. Ila shida ni moja siku ukisema bana sina. Hapo mada inabadilika inaonekana ww una roho mbaya. Husaidiagi watu yaani inasahaulika kabisa kwamba unapokuwa nacho huwa unajitoa.

Hii hali inakatisha tamaa inafanya nianze kufikiria kama hata ambavyonajitoaga huwa haithaminiwi kuna haja gani ya kuwa natoa. Kwanza msaada si lazima. Japo hata napotoaga huwa sitarajii return yeyote ila why siku ukisema huna inakuwa tatizo?
Si ni afadhali kuacha kabisa.....?
 
Kwenye kipato chako usisahau kupanga bajeti ya kusaidia ndugu, kwa kufanya hivyo roho haitakuwa ni yenye kulaumu.

Lakini hawa wanaosaidiwa na kubaki kulaumu pindi wasiposaidiwa, basi kuna shida miongoni mwao
 
Hili hawezi kufanya wengi wa watoa msaada hapa bongo wanatoa ili asifiwe au showoff kwa ndugu zake..
Ni kweli kila mmoja anataka yeye ndio awe mwamba , bila kujua ukizungukwa na ndugu maskini 9 wewe upo kwenye hatari ya kuwa wa 10 .
 
Hili hawezi kufanya wengi wa watoa msaada hapa bongo wanatoa ili asifiwe au showoff kwa ndugu zake..
Hakuna mtu takayependa upate kama yeye. Muda wote anataka uwe chini yake. Kwenye siasa hali ni mbaya zaidi. Kila msaada unaandamna na ma-kamera na ma-shukrani utadhani ni Mungu anaabudiwa. Hawataki kabisa kuwezesha wananchi wajitegemee. Na mbaya zaidi siku hizi wanasiasa wameacha kabisa kupanga maendeleo ya wananchi na muda wote wanautumia kwenye kamera eti kusikiliza kero za wananchi ili wananchi wawe tegemezi kwao muda wote wa maisha yao kama mbwa na binadamu.
 
Nilishajiapia sitakaa nibebe mzigo wa mtu yoyote hadi pale nitakapokuwa imara kiuchumi.

Unahangaika halafu unabeba mzigo wa muhangaikaji mwingine.

Ukiniomba msaada huwa napima uzito wa tatizo kama ni la kawaida nakupotezea labda iwe muhimu na hauna watu wa kukusaidia hapo nitakufikiria KIDOGO.

The truth is, NO BODY CARE ABOUT YOU.

Jipe umuhimu, hakikisha umesimama kiuchumi kisha extra unayopata ndiyo utoe.

Siyo mtu hauna kitu bado unabangaiza halafu unakomaa na ndugu ili uonekane una moyo wa huruma.

UTAKUFA MASIKINI!

BINADAMU SIYO KIUMBE CHA KUENDEKEZWA.

Sent from my SM-N950U1 using JamiiForums mobile app
 
Msaada sio haki yao ila ndio binadam walivyo hata ukiwasaidia bado watakunanga tu.
 
wengi wa wanao omba sana hawana akili ya utaftaji na ata ukimpa ramani ya kuipata hela bado huwa wanafeli

nakushauri msengenye huyo ane ombaomba aumie ili ajue kutafta chake na akome kuombaomba,,,, ipo siku atarudi kukushukuru kwa mtihani uliompa...

KAMWAMBIE by diamond na sarah wake.
 
Hiyo ndiyo shida?Si unanyamaza tu.Ndiyo ukubwa huo.Usianzishe tena uzi wa modeli hii.You won't be a@Troublemaker anymore!
 
Ni kweli kila mmoja anataka yeye ndio awe mwamba , bila kujua ukizungukwa na ndugu maskini 9 wewe upo kwenye hatari ya kuwa wa 10 .
Wengine hata ukiwaonesha njia wataendelea kukusumbua na hata kukushughulikia. Muuloze Pogba pamoja na Emanuel Adebayo watakuambia kuhusu kusaidia na kutaka kuinua ndugu.
 
Kwenye kipato chako usisahau kupanga bajeti ya kusaidia ndugu, kwa kufanya hivyo roho haitakuwa ni yenye kulaumu.

Lakini hawa wanaosaidiwa na kubaki kulaumu pindi wasiposaidiwa, basi kuna shida miongoni mwao
Asante fact.....
 
Hasa wanawake wana hiyo tabia sana. Utamsaidia mara 99, ukishindwa mara 1 tu zile 99 zinasahaulika unaonekana huna maana
 
Ukimsaidia mtu mara moja huo ni msada, Ukimsaidia mara ya pili huo ni ufadhiri, Ukimsaidia mara ya tatu huo ni wajibu ulio jipa mwenyewe.
 
Bado haujakua,ukiwa mkubwa utajua kuwa maneno ya masimango kuhusu wewe hayakupunguzii wala kukuongezea chochote.
 
Ukimsaidia mtu mara moja huo ni msada, Ukimsaidia mara ya pili huo ni ufadhiri, Ukimsaidia mara ya tatu huo ni wajibu ulio jipa mwenyewe.
😥😥😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…