Kutoka Mirembe
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 294
- 87
By the way mi mwenyew tokea mdogo nilikua naambiwa nisome sana ili nije kua na maisha mazur baadae, kauli ambayo nimekua nayo na imenifanya nisome kwa bidii na naamin maisha hayo mazur nitayapata tu inshaallah...
Mim nilisoma kupata maarifa ya kuniwezesha kupambana na changamoto za maisha.
Na ndio maana toka nimalize chuo 2010 sijawai enda omba kazi ata cheti sijakiangalia.
Elimu imenisaidia kufanya deal zangu binafsi na mambo yanaenda poa ningekuwa nimeajiriwa nisingekuwa apa nilipo maana deal moja tu ni sawa na mshahara wa muajiriwa wa zaidi ya mwaka.
Nasoma ili nije kumuoa dada yako
Nasoma ili nihamie mjini.
elimu za watu zinakuhusu nini?
acha kufuatilia mambo ya watu utaolewa bila mahari wewe
Nasoma ili nipate maaarifa na kutoa ujinga ili niweze jitawala .if to be employed is your reason you will work to build someone's dreams
Ha ha ha,kweli umerahisisha mkuu!Mbona jibu simple tu mkuu, nasoma ili nijue kusoma.
Kuna watu wamesona na ni masikini wa kutupa, na kuna watu hawajasoma na mambo yako swafi!.
Ha ha ha,kweli umerahisisha mkuu!
Kama ni hivyo,si form four ingetosha mkuu?
Ndipo ugomvi ulipo hapa.
Nikiwasoma,napata uelewa kwanini div 5 haziishi.
Nakwambia kweli mkuu, kwa kazi zetu na mazingira yetu, wengi wetu form 4 inatosha sana. Inategemea mleta uzi anaposema kusoma ana maanisha hadi kiwango gani.
Kwa kweli mkuu!
Mimi binafsi nilikaa miaka mingi baada ya kumaliza O level na kuji establish kimaisha na baadaye kuongezea kaji elimu kidogo.
Nashangaa humu watoto wanatoana macho kwa kutambiana vyuo.