Unasoma ILI IWEJE?

Unasoma ILI IWEJE?

Kutoka Mirembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
294
Reaction score
87
Hodi wana jukwaa,na habari za majukumu.
Najua watembeleaji wengi wa jukwaa hili ni wadau wa moja kwa moja wa elimu.
Sasa,naomba ku pose haka ka swali ka kutufikirisha kidogo:

JE,UNASOMA ILI IWE NINI?

Unapo jibu,jaribu kufikiri juu ya mfumo mzima wa elimu wa nchi yetu,na economic back ground ya wanafunzi wengi.
Naomba kuwasilisha.
 
ingekua vema ungejibu kwanza wewe mwenyew unasoma ili iweje ndo uulize maoni ya wana jukwaa...au we mwenyewe husomi au hujabahatika kusoma?...By the way mi mwenyew tokea mdogo nilikua naambiwa nisome sana ili nije kua na maisha mazur baadae, kauli ambayo nimekua nayo na imenifanya nisome kwa bidii na naamin maisha hayo mazur nitayapata tu inshaallah...
 
By the way mi mwenyew tokea mdogo nilikua naambiwa nisome sana ili nije kua na maisha mazur baadae, kauli ambayo nimekua nayo na imenifanya nisome kwa bidii na naamin maisha hayo mazur nitayapata tu inshaallah...

Ohoo,ahsante kwa mchango wako mkuu Goma Son
 
Last edited by a moderator:
ndoto hubadilika sana,hilo ni kawaida kwa wengi kutokana na changamoto za ufaulu,ajira,ugumu wa masomo,kwangu na kwa sasa nikupigania mapinduzi ya viwanda nchini na Afrika yote. Ndoto za zamani hazipo tena kwangu
 
Mim nilisoma kupata maarifa ya kuniwezesha kupambana na changamoto za maisha.

Na ndio maana toka nimalize chuo 2010 sijawai enda omba kazi ata cheti sijakiangalia.

Elimu imenisaidia kufanya deal zangu binafsi na mambo yanaenda poa ningekuwa nimeajiriwa nisingekuwa apa nilipo maana deal moja tu ni sawa na mshahara wa muajiriwa wa zaidi ya mwaka.
 
elimu za watu zinakuhusu nini?
acha kufuatilia mambo ya watu utaolewa bila mahari wewe
 
Mim nilisoma kupata maarifa ya kuniwezesha kupambana na changamoto za maisha.

Na ndio maana toka nimalize chuo 2010 sijawai enda omba kazi ata cheti sijakiangalia.

Elimu imenisaidia kufanya deal zangu binafsi na mambo yanaenda poa ningekuwa nimeajiriwa nisingekuwa apa nilipo maana deal moja tu ni sawa na mshahara wa muajiriwa wa zaidi ya mwaka.

What a great contribution!
Thank you Money Stunna
 
Last edited by a moderator:
Mbona jibu simple tu mkuu, nasoma ili nijue kusoma.

Kuna watu wamesona na ni masikini wa kutupa, na kuna watu hawajasoma na mambo yako swafi!.
 
Ha ha ha,kweli umerahisisha mkuu!
Kama ni hivyo,si form four ingetosha mkuu?
Ndipo ugomvi ulipo hapa.

Nakwambia kweli mkuu, kwa kazi zetu na mazingira yetu, wengi wetu form 4 inatosha sana. Inategemea mleta uzi anaposema kusoma ana maanisha hadi kiwango gani.
 
Kusoma ni asset Kama ilivyo asset zingine ambazo huchangia kuongeza kipato so waweza soma afu ukaajiriwa na huku unafanya mambo yako mengine na kuongeza kipato chako ili kupambana na ukali wa maisha .kifupi ni kwamba ajira ya kujiajiri au kuajiriwa kwa sasa inapaswa kuwa sehem ya kuongeza kipato na Sio kutegemea sehem moja peke yake.
 
Nakwambia kweli mkuu, kwa kazi zetu na mazingira yetu, wengi wetu form 4 inatosha sana. Inategemea mleta uzi anaposema kusoma ana maanisha hadi kiwango gani.

Kwa kweli mkuu!
Mimi binafsi nilikaa miaka mingi baada ya kumaliza O level na kuji establish kimaisha na baadaye kuongezea kaji elimu kidogo.
Nashangaa humu watoto wanatoana macho kwa kutambiana vyuo.
 
nasoma/nmesoma ili kupata maarifa mapya na kuweza kukabiliana na changamoto za maisha ikiwa ni pamoja na kuweza kujiendeleza kiuchumi...
 
Kwa kweli mkuu!
Mimi binafsi nilikaa miaka mingi baada ya kumaliza O level na kuji establish kimaisha na baadaye kuongezea kaji elimu kidogo.
Nashangaa humu watoto wanatoana macho kwa kutambiana vyuo.

Nakuelewa vizuri sana! Kwa mtazamo wangu, elimu yetu inatufundisha woga wa maisha badala ya kutufungua na kutuwezesha kukabiliana na changamoto za kila siku maishani.

Mfano mdogo tu, mtu mwenye elimu ya kawaida yuko ki halisia zaidi (more practical) kuliko mtu mwenye shule kubwa japo sio wote. Laiti tungepewa mtihani wa kuulizwa na watoto umefanya nini leo kazini, kuna watu wangeshundwa kujibu licha ya kwamba kila siku wanaenda kazini na wanalipwa mishahara mikubwa. Nasema watoto ili uweze kumweleza akuelewe unachokifanya kwa sababu mtu mzima ata jifanya amekuelewa hata kama kimsingi hujamshawishi kile unachokifanya unapokua kazini.

Mathalani, ma cashier kwenye ma benki wangelipwa pesa nyingi kwa sababu kazi yao inatambulika na kila mtu kuanzia aliyeenda shule hadi asiyejua kusoma. Kuna watu watakwambia sijui strategies, hawezi quantify kwa siku amefanya kitu gani tangible lakini mishahara ndio hiyo lumbesa.

Ndio maana tumekua na vijana wanaotafuta namna ya kupata mishahara mikubwa bila ya kujali kama watakua na uwezo wa kuzifanya hizo kazi zenyewe, mwisho wa siku ni frustration kibao.

Elimu ni nzuri sana kama itatafutwa kwa lengo la kuongeza uwezo na maarifa ya kukupatia ujasiri na maarifa ya kutatua matatizo yako na yanayoizunguka jamii kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom