Jebel
JF-Expert Member
- Jul 10, 2021
- 386
- 2,615
MIEZI 3 KWENYE BIASHARA YA SPARE ZA PIKIPIKI FAIDA NA CHANGAMOTO ZAKE
Salamu,
Baada kuiwazia sana biashara hii nikaona si vibaya nikaweka vimillioni kadhaa ili nione kama kweli iko kama isemwavyo, si unajua utamu wa ngoma.......
Kituo cha kwanza nikatinga wizara ya JF ili kupekua makaburasha kadhaa nione kama kuna lolote la kujifunza huko.
Kituo cha pili nikaingia jamhuri ya FB na IG kuona pia kama naweza kupata lolote. Kweli mengi niliyapata.
Kituo cha tatu nikacheki na fundi pikipiki rafiki yangu sana naye bila inda akanipatia ABC za uchuuzi huu.
Baada ya kukusanya taarifa nilizoona zinatosha kabisa ikabidi nitafute fremu tayari kwa kuanza shughuli.
Eneo nililofungua biashara ni wilaya X mkoani. Sababu niliangalia sehemu ambayo bado hakuna maduka mengi ya jumla makubwa makubwa.
Baada ya kumaliza hatua za kulipia pango na kumpata muhudumu ilinibidi nikamate chuma LORI LA MAFUTA maarufu kama TANK kuingia jijini Dar. Binafsi napendelea kupanda Lori kuliko bus, kikubwa liwe Tank empty au chanja empty na liwe Scania au Benz kwa ajili ya comfortability.
Niliingia Dar mwezi May kwa mawasiliano ya jamaa wanajiita ........(Naomba nisiwataje) Niliwapata FB wakidai kwa "ntu" anayeanza biashara hii wanampatia darasa la kutosha juu ya uendeshaji wake. Nikaona hawa ndo watu sasa wa kuanza nao.
NB kama ningejua ningekubali gharama za kumlipia nauli fundi kutoka mkoani nikaja naye Dar. Hapa nilifanya mistake kubwa sana kuja mwenyewe na kuwaamini Wafanyabishara wa Kibongo!
Mzigo wa kwanza nilichukua spare za 20Million ikiwa ni jumla ya items karibu 200. Baada ya kufika ofsini kwao aliitwa kijana mmoja akanifanyia order ya spare muhimu zinazotoka sana za pikipiki aina ya SanLg na Kinglion kwani ndizo pikipiki zilizotawala sehemu nilipofungua biashara. Lakini pia nilichukua mzigo wa spare za BM na TVS wa karibu 3M.
CHANGAMOTO 1
Kulingana na ukubwa wa mzigo na items kuwa nyingi nisingeweza kusubiria kuhakikisha kila kitu kama kimefungwa hivyo spares nyingi hazikufungwa kama nilivyofanya malipo. Naomba nifafanue hapa, baadhi ya spare hawakuwa nazo dukani kwao hivyo waliniomba kuwapa mda wa kutosha wa kuzikusanya kwa ahadi ya kufunga mzigo wote na kisha kuuleta sehemu nitakapoupakilia mimi kwa gharama zao. Hivyo baada ya kufanya malipo nilienda kufanta service ya gari yangu ambayo niliitumia kuleta mzigo kutoka Dar ni Velfire hivyo mzigo ulitosha vema. Gari hii ipo Dar special kwa kukodiwa.
CHANGAMOTO 2
Kutokana na ugeni wa biashara hii nilijikuta nauziwa spare kwa bei za juu sana kiasi cha kushindwa kuuza baadhi ya spare kwa mfano Tank la mafuta niliuziwa 60Elfu kufika mkoani bei yake ni 50 hadi 45!Elfu. Hapa ndo maana nasema ni vema ningeenda na fundi anayejua bei ningeepuka hii kadhia ya bei za juu sana.
CHANGAMOTO 3
Kuuziwa spare ambazo wengi hawazipendi, spare za bei ya chini na quality ya chini sana. Kwa mfano spare ambazo wateja wengi wanazipenda ni company ya SLL lakini mimi hizi niliwekewa kidogo sana zaidi niliwekewa makampuni mengine ambayo wateja wengi hawayapendi.
NB hizi spare za company zisizo na majina ukizinunua kwa bei ya chini huwa zinatoa faida tamu sana kuliko spare za company kama SLL. Mfano unaweza kununua spare A ya SLL kwa Tsh4000 bei ya jumla na kuiuza Tsh5000 rejareja halafu spare hiyohiyo A ya compareX ukaiununua kwa Tsh2000 bei ya jumla kuiuza Tsh5000 rejareja.
CHANGAMOTO 4
Asikudanganye mtu biashara ya spare za pikipiki bila kuwa na fundi mzuri kuuza spare utasubiri sana. Yaani kabla hujafungua biashara hii hatua chanzi ni kutafuta fundi mzuri kwanza atakayefanyia kazi ofsini kwako. Binafsi nilifungua bila fundi na changamoto hii imeniotesha joto la jiwe. Kwa bahati tangu nipate fundi mambo yanaenda vema kabisa.
FAIDA ZA BIASHARA HII
Ni kweli kila biashara ina changamoto lakini biashara hii ya spare nikifanya comparison ba biashara zangu nyingine za usafirishaji abiria na biashara ya kuweka mazao stock binafsi naona hii ina unafuu sana.
Kwanza spare hazi expire wala kubunguliwa badala yake kila siku zinapanda bei.
Tunachokijua: biashara ya spare za pikipiki ukiuza laki2 una faida ya hadi elfu 80! Yaani zaidi ya 50%.
Binafsi nimeamua kuingia mazima katika biashara hii nataka niweke 80M kwani naona ndani ya miezi 3 siyo haba. Kwa 20M niliyoanza nayo walau pesa ya kula na kuchepuka kidogo haikosekani!!!
HITIMISHO
Kama kuna mtu ambaye angependa kuingia kwenye biashara hii ningemshauri asiogope badala yake ajitahidi kufuata ushauri nilioutoa humu yaani
1. Ajitahidi kupata sehemu sahihi ya kuchukulia mzigo
2. Apate fundi mzuri
3. Anunue spare kwa bei nzuri ili auze kwa bei nzuri pia
4. Fremu iwe sehemu yenye mzunguko mzuri
5. Kuwa na spare zinazotoka sana. Hizi mafundi wanazifahamu vema
MWISHO KWA YEYOTE ANAYETAKA USHAURI KARIBU INBOX NITAKUJIBU SWALI LOLOTE KADIRI YA UELEWA WANGU
Mungu ibariki Tanzania ila usiibariki CC???