Unataka Kupima kama huyo Mpenzi wako ni Wife Material? Mpeleke kwa Mama Ntilie, akisumbua mhudumu mara 3 kwa sababu zinazovumilika PIGA CHINI!

Nipo zangu kwenye mgahawa, napata menu, halafu kuna binti naye yupo hapa. YAAANI mwanamke msumbufu kwenye kuagiza chakula mpaka unaanza kujiuliza huyo jamaa wake huko nyumbani anapitia nini.

Akaletewa wali na nyama. Lakini haikuchukua sekunde nyingi, akaanza malalamiko—nyama ina mafuta. Mhudumu, kwa ustaarabu wake, akambadilishia. Baada ya kula vijiko viwili, akaita mhudumu tena: "Samahani, naomba chumvi, lakini pia huu wali una kiini." Ikumbukwe, sisi wengine tunakula wali huo huo na upo sawa tu.

Bado mambo hayajaisha. Akaagiza soda. Soda imefuka kidogo, akalalamika: "Hii haina ule unaridi nilioutegemea." Wahudumu wakamweleza kwa upole kuwa cha baridi sana ni juisi ya matunda, maana imekaa muda mrefu kwenye friji. Badala ya kuelewa, akaanza kubwabwaja juu ya hatari ya kuumwa tumbo kwa kunywa juisi hiyo. Ikumbukwe, sisi wengine tunakunywa juisi hiyo hiyo na hakuna anayelia.

Kwa nilichoshuhudia hapa, nimepata litmus test matata kwa wanaopanga kujivutia jiko ndani. Unataka kujua huyo mwanamke kama mtawezana? Mpeleke kwa Mama Ntilie. Kama ataita muhudumu mara tatu kwa mambo madogomadogo ambayo yanaweza kuvumilika, tambua kuwa huko mbele kuna safari ngumu. Lakini kama anaweza kula kilichopo bila visingizio vya kila dakika, basi pengine huyo anaweza kuwa chaguo sahihi.

Maisha siyo Instagram. Uvumilivu kwa mambo madogo huakisi uwezo wa kuvumilia changamoto kubwa. Kama mwanamke anaweza kufanya wahudumu wakakimbizana kwa amri zake zisizoisha kwa mlo mmoja, vipi itakavyokuwa kwenye ndoa? Kaka, zingatia.
Kwenye suala la msosi ni kweli kabisa wanawake wapunguze kujishaua. Wenyewe wanafikiria ndo usister du kumbe kero tu. Mimi huyu mtoto wa mama mkwe mwanzoni wakati tunajuana alikua na tabia inayofanana na iyo. Unakuta tumeenda restaurant anaagiza chakula au kinywaji halafu anagusa kidogo tu eti ndo ameshiba, nikampa onyo kali sana nikamwambia mimi hela siokoti natafuta kwa jasho kwaiyo kama tukienda sehemu kama haujisikii kula au kunywa chochote basi usiagize kabisa hicho chakula unachojishaua kula kuna masikini wanakikosa. Mpaka leo hajawahi kurudia tena huo utoto
 
Asa kiongozi kama chakula kingi uwa tuna pack take away siachi Ata kuku😹
 
Nipo zangu kwenye mgahawa, napata menu, halafu kuna binti naye yupo hapa. YAAANI mwanamke msumbufu kwenye kuagiza chakula mpaka unaanza kujiuliza huyo jamaa wake huko nyumbani anapitia nini.

Akaletewa wali na nyama. Lakini haikuchukua sekunde nyingi, akaanza malalamiko—nyama ina mafuta. Mhudumu, kwa ustaarabu wake, akambadilishia. Baada ya kula vijiko viwili, akaita mhudumu tena: "Samahani, naomba chumvi, lakini pia huu wali una kiini." Ikumbukwe, sisi wengine tunakula wali huo huo na upo sawa tu.

Bado mambo hayajaisha. Akaagiza soda. Soda imefuka kidogo, akalalamika: "Hii haina ule unaridi nilioutegemea." Wahudumu wakamweleza kwa upole kuwa cha baridi sana ni juisi ya matunda, maana imekaa muda mrefu kwenye friji. Badala ya kuelewa, akaanza kubwabwaja juu ya hatari ya kuumwa tumbo kwa kunywa juisi hiyo. Ikumbukwe, sisi wengine tunakunywa juisi hiyo hiyo na hakuna anayelia.

Kwa nilichoshuhudia hapa, nimepata litmus test matata kwa wanaopanga kujivutia jiko ndani. Unataka kujua huyo mwanamke kama mtawezana? Mpeleke kwa Mama Ntilie. Kama ataita muhudumu mara tatu kwa mambo madogomadogo ambayo yanaweza kuvumilika, tambua kuwa huko mbele kuna safari ngumu. Lakini kama anaweza kula kilichopo bila visingizio vya kila dakika, basi pengine huyo anaweza kuwa chaguo sahihi.

Maisha siyo Instagram. Uvumilivu kwa mambo madogo huakisi uwezo wa kuvumilia changamoto kubwa. Kama mwanamke anaweza kufanya wahudumu wakakimbizana kwa amri zake zisizoisha kwa mlo mmoja, vipi itakavyokuwa kwenye ndoa? Kaka, zingatia.
Duh umeongea kama nabii mkuu
 
Kiongozi sio Kila mpenda cappuccino alitaka aolewe na mzungu what a backward thinking na ambae atanioa ajue coffee dates lazima that what I like ā™„ļøšŸ˜¹
... you draw your line and he draws his line, the one who ignores his/her line is the one really in LOVE!
🄰
 
Back
Top Bottom