Unataka Kupima kama huyo Mpenzi wako ni Wife Material? Mpeleke kwa Mama Ntilie, akisumbua mhudumu mara 3 kwa sababu zinazovumilika PIGA CHINI!

Unataka Kupima kama huyo Mpenzi wako ni Wife Material? Mpeleke kwa Mama Ntilie, akisumbua mhudumu mara 3 kwa sababu zinazovumilika PIGA CHINI!

Msiwe mnapenda kuwapa watoto wa watu mitihani ya roho mbaya ili kuprove point kuwa anafaa au hafai.

Kwahiyo mtakuwa mnakula kwa mama ntilie au?

Why sasa iwe kipimo cha kumpimia mke in the first place kama sio uchawi.
 
What has to do with love?? Sijakupata kabisa Yan mim kukosoa kitu ndo iwe sababu ya kuachika kheee umalaika gan huo niliokua nao jaman

Wanaume wengi hamjui kujudge chakula ni wachache sana wanafanya Ivo ila Kwa wanawake Hilo ni kawaida sana Kwan kusema sili nyama ya mafuta Kuna tatizo? Na hii Hali ya hewa upewe soda ya moto itashuka kweli? Juice za kutengeneza hazina usalama ndio tumeona kwenye mitandao wanavoosha miguu kwenye juice ndo watengeneze sijaona baya alilofanya
 
😁😁😁
Mimi usumbufu wangu unakuwaga kwenye namna ya kushika chupa ya soda mhudumu/muuza vinywaji anaponiletea.

Sipendi ashike shingo ya chupa.

Upande wa chakula nitamsumbua kwenye kufuta meza kabla hajaleta chakula.

Hili nalo ni tatizo?
 
Wanawake wengi wapo hvyo wanapokuwaga migahawani,mke wangu nae yupo hvyo na kweli nyumban panawaka moto kabla ya mwez wa nne nitakuwa nimeshamkimbia

Kuna demu mmoja aliwah niambia hawez kula mgahawan,ni bora ajipikie,anasema huwa hajisikii vizuri kula chakula kilichopikwa na mwanamke mwingine ambae hajamzoea
Sasa unamkimbia unakwenda wapi?
Unamwachia nani? 😁😁😹
 
Nipo zangu kwenye mgahawa, napata menu, halafu kuna binti naye yupo hapa. YAAANI mwanamke msumbufu kwenye kuagiza chakula mpaka unaanza kujiuliza huyo jamaa wake huko nyumbani anapitia nini.

Akaletewa wali na nyama. Lakini haikuchukua sekunde nyingi, akaanza malalamiko—nyama ina mafuta. Mhudumu, kwa ustaarabu wake, akambadilishia. Baada ya kula vijiko viwili, akaita mhudumu tena: "Samahani, naomba chumvi, lakini pia huu wali una kiini." Ikumbukwe, sisi wengine tunakula wali huo huo na upo sawa tu.

Bado mambo hayajaisha. Akaagiza soda. Soda imefuka kidogo, akalalamika: "Hii haina ule unaridi nilioutegemea." Wahudumu wakamweleza kwa upole kuwa cha baridi sana ni juisi ya matunda, maana imekaa muda mrefu kwenye friji. Badala ya kuelewa, akaanza kubwabwaja juu ya hatari ya kuumwa tumbo kwa kunywa juisi hiyo. Ikumbukwe, sisi wengine tunakunywa juisi hiyo hiyo na hakuna anayelia.

Kwa nilichoshuhudia hapa, nimepata litmus test matata kwa wanaopanga kujivutia jiko ndani. Unataka kujua huyo mwanamke kama mtawezana? Mpeleke kwa Mama Ntilie. Kama ataita muhudumu mara tatu kwa mambo madogomadogo ambayo yanaweza kuvumilika, tambua kuwa huko mbele kuna safari ngumu. Lakini kama anaweza kula kilichopo bila visingizio vya kila dakika, basi pengine huyo anaweza kuwa chaguo sahihi.

Maisha siyo Instagram. Uvumilivu kwa mambo madogo huakisi uwezo wa kuvumilia changamoto kubwa. Kama mwanamke anaweza kufanya wahudumu wakakimbizana kwa amri zake zisizoisha kwa mlo mmoja, vipi itakavyokuwa kwenye ndoa? Kaka, zingatia.
Noted,nitaisave hii kwenye diary...
 
😁😁😁
Mimi usumbufu wangu unakuwaga kwenye namna ya kushika chupa ya soda mhudumu/muuza vinywaji anaponiletea.

Sipendi ashike shingo ya chupa.

Upande wa chakula nitamsumbua kwenye kufuta meza kabla hajaleta chakula.

Hili nalo ni tatizo?
Hayo sio matatizo, ila Hilo la kushika chupa ya soda Bora utembee na tissue Yako uwe unafuta soda, ukilalamika watasema unajishaua😂
 
What has to do with love?? Sijakupata kabisa Yan mim kukosoa kitu ndo iwe sababu ya kuachika kheee umalaika gan huo niliokua nao jaman
Nikikupeleka kwa wakwe utaanza kumsumbua mama yangu maana ushaonekana ni mtu wa high maintenance, usije kusema bimdashi anapika mchuzi nyanya zinaelea wakati sisi ndio tunavyokulaga
 
Ndio
Wanaume wengi hamjui kujudge chakula ni wachache sana wanafanya Ivo ila Kwa wanawake Hilo ni kawaida sana Kwan kusema sili nyama ya mafuta Kuna tatizo? Na hii Hali ya hewa upewe soda ya moto itashuka kweli? Juice za kutengeneza hazina usalama ndio tumeona kwenye mitandao wanavoosha miguu kwenye juice ndo watengeneze sijaona baya alilofanya
Ndio uanze kusumbua watu kwa chakula cha 1500 kweli?
 
Of course, mwanaume Sio kama kuku anayerudi bandani kwa majira ya jua kuzama
Muwe mnasema tu ukweli kwamba mnataka wanawake watakaowavumilia tabia zenu mbovu kama ulevi na uasherati msiseme mambo madogo madogo
 
Back
Top Bottom