nakwede97 Anastasia21 Xi Jinping Natafuta Ajira Extrovert Zemanda Fanton Mahal Melancholic mm binafsi nina theory yangu, ukiacha swala la kumshirikisha Mungu ili mwanaume upate wife material, hii ni njia ya kum-test mdada kama ni wife material, hii test wanawake wengi sana huwa wanafeli
Generosity test:
Mwanaume unamuomba girlfriend wako, au hata mdada ambae una mpango wa kumtongoza, unamuomba kitu kidogo sana, like unamuomba akununulie andazi, au lunch. Simaanishi mwanaume ndo uwe marioo, jukumu la ku-provide linakua palepale, ila unamuomba halafu unaangalia reaction yake..mara nyingi it's aidha akunyime au akupe huku analalamika
Hii test ni noma sana, many women wanafeli hii test, ndo utajua girlfriend wako ni mtu wa namna gani, like hata ukimuoa hatopenda wageni, na ndugu wa mume from start, ataona wanammalizia chakula..
Hii test pia inaonesha her interest level kwa mwanaume, mwanamke asiekupenda hawezi kubali ule vyake, most of times na hii test utagundua kumbe girlfriend ulienae ni mchoyo/golddigger/ kwako kajiegesha tu
NB: Mwanaume ukitaka wife material hakikisha na wewe ni husband material, sio unaotaka wife material ila unachepuka, huhudumii familia, unanyanyasa mke na watoto, etc