MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Pendekezo la Mradi yaani "Grant/Business Proposal" ni andiko linaloonyesha hitaji (need), fursa (opportunity), au tatizo (problem) lenye kuhitaji kuchuliwa hatua. Mmiliki wa tatizo, fursa au hitaji anaweza kuwa Taasisi, Kampuni, Jamii au hata mtu mmoja mmoja. Kupitia Pendekezo la Mradi, muandaaji huweza kuainisha mpango (a detailed plan) unaohitajika ili kutatua tatizo (ikiwa kuna tatizo) , kufaidika na fursa (ikiwa suala ni fursa) au kukidhi hitaji (ikiwa suala ni hitaji). Mbali na mpango, muandaaji pia anapaswa kuainisha gharama za utekelezaji wa mradi, matokeo yanayotarajiwa kutokea baada ya utekelezaji wa Mradi, na makadirio ya muda wa utekelezaji wa Mradi.
Uandaaji wa Pendekezo la Mradi ni miongoni mwa njia za utafutaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kwa Taasisi, Kampuni na hata kwa mtu mmoja mmoja. Pendekezo zuri la Mradi yaani "Successful Grant/Business Proposal" hujengwa katika misingi mikuu miwili, ambayo ni;
- Kuijua hadhira yako ambayo ni; wafadhili au wadau wa mradi wako.
- Kuandika kile ambacho hadhira yako inataka kujua na si kile unachojua wewe.
Hivyo basi pindi uandaapo Pendekezo lako la Mradi zingatia sekta ambayo mradi wako umejikita, na uandishi wako ujikite katika mtazamo (perspective) wa hao unaowaandikia pendekezo hilo. Kwa mfano; utafanya makosa endapo utatumia misamiati ya kisheria katika uandaaji wa pendekezo la mradi wa mazingira au ufanye kinyume chake.
Kujua hadhira yako inataka nini katika pendekezo lako la Mradi, Wito wa Uwasilishaji wa Mapendekezo ya Miradi yaani "Request for Proposals" ni nyaraka muhimu kwako itakayokujulisha juu ya nini mfadhili anataka kujua kutoka kwako. Nyaraka hii itaweza kukuonyesha maudhui ya mradi "thematic areas", aina ya miradi inayopendekezwa kwa kila "thematic area". Haiishii hapo nyaraka hii itaweza pia kukuonyesha bajeti ya programu (Ufafanuzi: Programu ni mjumuiko wa miradi mbalimbali yenye kushabihiana malengo) mbali na bajeti ya programu pia nyaraka hii itakuonyesha kiasi cha chini kabisa kuomba kwa ajili ya pendekezo lako (Award Floor) na kiasi cha juu kuomba (Award Ceiling) kwa pendekezo. Pia nyaraka hii itakuonyesha namna ya kuwasilisha pendekezolako, muda wa uwasilishaji wa pendekezo lako n.k
OMAR MSONGA (BA. PPM &CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA