Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Mimi binafsi huwa naendesha kale katairi nikiwa nimesimama yaani sio kwa kuweka magoti sakafuni

Sasa watu huwa wananiangalia wanasema kwani hilo tumbo lako lina misuli ya chuma??
Hahahahahaha mazoezi raha aisee
 
Fanya mazoezi haya kupata six packs haraka au kuondoa nyama uzembe ukiwa nyumbani bila kifaa chochote bila ya kwenda gym.
 
Fanya mazoezi haya kuondoa mafuta yasiohitajika mwilini, kuondoa nyama uzembe na kupata six packs haraka ukiwa nyumbani bila kwenda gym
 
Nitakupm namba mkuu,ile isiwe ile wanaita mauaji unashindia maji tupu jioni ndo unakunywa glass moja ya maziwa kesho yake maji tupu mpk asubuhi nyingine hapana!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wapenda kula utawajua tuu[emoji12]
 
Nami nitoe ushuhuda
Nimepungua kwa mazoezi ila kwakweli mazoezi kipaji
Kuna siku nakuwa mvivu sifanyi kabisa naweza kukaa siku mbili hadi tatu nakumbuka nilikotoka narudi katika mstari.
Ila yanahitaji moyo
Mimi huwa nafanya usiku kabla sijalala mana asubuhi na nakuwa mvivu plus sitaki kuamka mapema au kukwepa kuchelewa kuamka hivo kuacha kufanya ili uwahi mishe zingine plus hili baridi la sasa hivi.
Nilianza na kila zoezi *20 nikafika 30 sasa naenda mpaka 80 lengo nataka nifike 100 kila zoezi.
Nafanya mazoezi ya aina 15 tofauti nimejifunzia You tube.
 
Mimi tangu nifilisike mwili umeisha wenyewe na nime kua na tumbo flati. Kumbe umasikini nao ni mzuri jmn
 
kwa mfano mkienda sehemu ya huduma watu wawili mwenye kitambi na mwingine flat lazima ataanza kuhudumiwa mwenye kitambi na aliye flat atafuata baadae.
Utakuta wahudumu wanakuita kwa unyenyekevu"Karibu Boss,tunaomba tukuhudumie" sasa hii favour ndio inayonifanya niache kujichosha au kujishindisha na njaa kwa ajili ya kukiondoa kitambi.
Athari za umasikini ziko wazi sana kwenye jamii yetu
 
Uzi mzuri sana ku motivate wanaoanza mazoezi na ambao wanasusa susa kwenye mazoezi.
Kweli mazoezi yanataka commitment ya kweli nq iwe sehemu ya maisha yako. Me nilikuwa Bonge nikaanza kwenda gym bila kufata ushauri nikawa nanyanyua mavyuma nanogewa si unajua ile mambo za vijana, baada ya mwezi nikaona nime gain 5 more kg. Nikaacha mazoezi nikapiga story na jamaa yangu trainer akaniambia usingeacha ila usifate mkumbo kunyanyua uzito mkubwa kachuma kadogo tu, cardio kwa sana na diet ndo kila kitu.


Baada ya muda sasa nimeamua diet na mazoezi iwe sehemu ya maisha yangu kila siku asubuhi nakimbia kwenye kilima kwa nusu saa. Nikimalizia nafanya cardio na mazoezi ya kutengemeza abs. Almost lisaa kwa mazoezi yote kuanzia saa 04:45 am hadi 06:00 am. Na feel good nikifanya mazoezi hata ukienda haja wajisikia poa sana sio kama zamani patapatapat, pia mazoezi yana boost Libido and confidence.
 
Daah kuna zoezi niliangalia youtube linafanana kidogo na hilo la pili ila lenyewe unanyanyua magoti unaleta tumboni. Siku ya kwanza nimefanya siku ya pili sasa maumivu chini ya kitovu utasema kizazi kinachomoka. Bado najifikiria niendelee au niache. Ngoja nisubscribe hapa kwanza
Ungeendelea ndo mishipa inatanuka!
 
Back
Top Bottom