Ulweso
JF-Expert Member
- May 24, 2016
- 23,111
- 28,020
Kukaa mbali mbali ni nzuri sana tena sanaHakika ni ngumu sana mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kukaa mbali mbali ni nzuri sana tena sanaHakika ni ngumu sana mkuu
Absolutely trueKukaa mbali mbali ni nzuri sana tena sana
Gambe gambe gambe.....daaah, umenikumbusha mbali sana mkuu enzi zanguHapa penyewe namsubiri tuje tuanze kugambika maana bila yeye hazishukagi kabisa😂😂😂😂😂😂😂😂
Ndio hivyo mkuu, rafiki jenga naye hata 30 kilometers awayRafiki yangu alitaka kunikatia kiwanja chacke kama one eka hv kwa gharama ndogo sana ili tuu tujenge na kuish jirani woote. Nlipokaa nkafikiria na kuyasikiliza maini yangu aisee nilichomoa aisee. Na saiv mtaa anaoish yeye na mm ni mbali kabisaaa
Rais Samia analeta maendeleo kila kona ya Nchi. Hakika huyu mama ni zawadi ya Mungu kwa watanzania.Samia anajenga stiglers gorge ambayo ilimshinda Mjerumani miaka hiyo wakati bado anaitawala Tanganyika kwa mabavu
Hii n kweli aseeHakunaga urafiki wa milele, kwanza hilo tulijue.. Rafiki yako wa primary utampoteza ukihamia secondary, rafiki wa mtaani kuna muda utampoteza, rafiki wa o level, utampoteza rafiki wa a level utampoteza, rafiki wa chuo utampoteza, hata wa kazini pia utakuja mpoteza, wote tutakuwa tumeexperience hili jambo.. Ukitoka hatua moja kwenda nyingine unapoteza watu, mkiachana katika harakat za maisha, kila mtu akashika njia yake lazima upoteze rafiki pia.
Duuuh, hii yako sasa ni too much mkuuMm hata nnapopanga chumba/nyumba hua naenda kupanga sehemu ambayo hakuna anaenijua na nikigundua mtaa huo kuna mtyu ananijua basi nabadili njia ya kupita.
Wakati nasoma, nilikua najitahd nikae na roommate ambao hatujuan kabisa. Siwez kukaa na rafiki angu room moja yaan kwny usajili nikiona tumeongozana na rafki yangu kwny folen bas ntafanya ujanja ujanja niondoke kwanza ili yy asajiliwe afu mm ntakuja sajiliwa bdae.
Hata nikiwa naenda kula mgahawan/cafe, kabla cjaingia hua naangalia je kuna mtu ananijua humu?? Nikimwona bas naenda zangu kula kwny cafe nyngne.
Inshort spend bugdha bugdha na kujuana juana sana.
Marafiki mlioshibana mnaweza kama hivyo, kununua viwanja, kushauriana n.k. mkipata wenza, hawatakubali upate ushauri huo tena ilhali wao wapo, na kunakuwa na wivu, kwamba unamjali rafiki zaidi.Good afternoon JamiiForums.
Je, unataka urafiki wenu uendelee kudumu miaka na miaka? Basi usijenge nyumba jirani na yule "best friend" yako. Usifikiri mkijenga majirani ndio mtadumisha urafiki wenu mkuu. Hapana kwa sababu kuu moja kwamba, wewe na yeye mnaweza kuwa "best friends" lakini wake zenu wasiwe mtu na shoga yake. Umenipata mkuu? Umenisoma mzee baba?
Hii imekaa hivi, Pipa na Mfuniko ni marafiki wa muda mrefu sana. Walikutana kazini au zamani walikuwa wanakaa mtaa mmoja na kucheza wote ile michezo ya kitoto. Kuna uwezekano mkubwa pia hata labda Pipa na Mfuniko walikutana chuoni UDSM wakitokea shule tofauti za secondary, lakini walipokuwa chuo walikuwa wanafanya mambo yao kwa pamoja mpaka wakawa marafiki.
Inawezekana walikuwa kozi moja, walikuwa discussions group moja, walikuwa wanakunywa beer wote siku za weekend na kufukuzia pisi kali za chuo. In sort itoshe kusema kwamba, Pipa na Mfuniko ni marafiki wa kufa na kuzikana.
Punde baada ya kuhitimu elimu ya juu mwaka 2013 walikula msoto mwaka mmoja na hatimaye kupata kazi kampuni tofauti Dar lakini bado wakawa wana-hangout pamoja.
Kosa ambalo huyu Pipa na rafiki yake mfuniko wanaweza kulifanya likaja kuua urafiki wao ni pale ambapo wataamua wote kwenda kununua kiwanja sehemu moja. Hahahahaaa, that's a fatal mistake my friend. Usinunue kiwanja kisha ukajenga na kuishi jirani na rafiki yako mkuu kwa maana nyie mnaweza mkawa maswahiba lakini wake zenu wasishibane.
Kama pipa amenunua kiwanja Boko, basi mfuniko ajitahidi aende akanunue huuuuuko Kibamba ili kuongeza ladha ya urafiki. Kama mnakaa Arusha, wewe ukipanga nyumba Njiro, basi rafiki yako yeye akakae Sakina. Msikae karibu kama kweli mnataka urafiki wenu uendelee kudumu.
Kuna kitu kimoja ambacho kimejificha katika urafiki nahisi watu wengi hawakifahamu. Urafiki ni mtamu kama mnaonana mara moja moja. Hii ndio siri kubwa na urafiki mtamu. Ukikaa muda mrefu haujaonana na mtu ndio mnakuwa na mambo mengi ya kusimuliana, na hapa ndio utasikia "aisee, Pipa alikuja kikazi Dar akitokea Mwanza, tulipiga story mpakaa saa saba usiku". Kwanini wapige story mpaka usiku wa manane? Sababu ni moja tu, hawajaonana muda mrefu.
Urafiki wa kuonana kila wakati wa kuwa majirani ipo siku wake au watoto zenu watawagombanisha. Mdogo wangu uliyeanza kazi hapa juzi juzi tu, hivi unawajua wanawake au unawasikia? Hivi unafikiri wahenga waliposema kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzio waliokosea? Wewe (Pipa) unaweza ukanunua sofa mpya lakini rafiki yako (Mfuniko) hajabadili viti mwaka wa tano sasa.
Unafikiri kinachofuata ni nini kama sio shemeji yako (mke wa Mfuniko) kumnunia mkeo? Mama watoto wako amepika vizuri siku ya X-mass, lakini kwa best yako pamedorora, ni nini kitafuata hapa kama sio beef?
Wake zetu tunawapenda sana, lakini wao kwa wao wasipoiva chungu kimoja sidhani kama mtu na best yake wataendelea kuchekeana kama zamani, tena mbaya zaidi ukute mke wa mfuniko anafanya kazi Bank lakini yule wa Pipa yeye ni mama wa nyumbani, mbona urafiki huo wa tangia utotoni/chuoni utaingia doa.
Kama unataka urafiki wenu uendelee kudumu muda mrefu, usijiroge ukajenga eneo moja na best friend yako, ooooho sasa wewe jifanye mjuaji, kuna siku utaukumbuka huu ushauri wangu.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Yes, that's very true brotherMarafiki mlioshibana mnaweza kama hivyo, kununua viwanja, kushauriana n.k. mkipata wenza, hawatakubali upate ushauri huo tena ilhali wao wapo, na kunakuwa na wivu, kwamba unamjali rafiki zaidi.
Viongozi wa bara la Ulaya na Asia kama vile Waziri mkuu wa India Narendra anamkubali sana Rais SamiaMama yetu Rais Samia ametoa pesa nyingi sana kwa ajili ya miradi mizuri ya maendeleo. Mungu mpe afya njema shujaa huyu
Mbona chadema kama vile wanapanic? Ina maana hawapendi maendeleo anayoleta Rais Samia?Viongozi wa bara la Ulaya na Asia kama vile Waziri mkuu wa India Narendra anamkubali sana Rais Samia
Tunashukuru Tanzania tumepata Rais Mzalendo anayeipenda Nchi yake Samia oooyeeeeeeMbona chadema kama vile wanapanic? Ina maana hawapendi maendeleo anayoleta Rais Samia?
Rais Samia amejua kutupigania Watanzania Wish you all the best Madam PresidentTunashukuru Tanzania tumepata Rais Mzalendo anayeipenda Nchi yake Samia oooyeeeeee