MIHAYO1710
Member
- Apr 7, 2018
- 23
- 59
UNGEPENDA KUWA ZAIDI YA BINADAMU WA KAWAIDA? WATOTO WA MUNGU NI MIUNGU!
"A KINGDOM WHERE MANKIND BECOME gODS: A RENAISSANCE"
Amani na Salama 🙏🙏🙏
Ninao ujasiri mkubwa, na furaha ya ajabu kukufahamisha HABARI njama za Ufalme wa Mungu!
👉Ni adhima, shauku, kiu na ndoto ya kila binadamu Mwenye akili timamu, kuishi maisha ya viwango vya juu zaidi, yaan maisha yanayovuka mipaka ya kawaida ya ubinadamu!!
👉Ili kutimiza adhima, ndoto na kiu hiyo, watu hutafuta mlango wa kutokea. Milango hiyo ni kama vile kutafuta Mali, elimu, madaraka, vyeo, teknolojia na tafiti! Wengine huwekeza sana Kwenye mambo ya nguvu za giza, na Dini! Lengo lao ni Moja, kujaribu kuishi maisha ya kiwango Cha juu zaidi kuliko wanadamu wengine!!
(Umewahi kusikia Kuna watu Wana shauku ya kutaka kuhama duniani, waanzishe makazi sehemu nyingine, kama vile sayari ya Mars?)
👉Maisha ya juu, maana yake ni kuwa na uwezo, nguvu na hata ujuzi zaidi ya ubinadamu wa kawaida! Hata kuweza kushangaza wengine!!
MIFANO
1. Kushangaza watu Kwa nguvu za uchawi
Matendo ya Mitume 8:9-11
[9]Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya UCHAWI katika mji ule, AKIWASHANGAZA watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu MKUBWA.
[10]Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
[11]Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.
👉Huyu simoni, aliheshimiwa na watu wote Kwa sababu tu alikuwa na maarifa ya kichawi.
2. Kushangaza watu Kwa sababu ya hekima kubwa!
👉Ndiyo, Kuna watu Hapa duniani ufahamu wao Huwa uko mbele na juu sana. Kazi ya wanadamu wengine hubaki kustaajabia/kuishangaa hekima hiyo!
👉Watu walishangaa UKUU wa hekima ya Yesu akiwa Bado kijana mdogo tu.
Luka 2:47
[47]Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.
👉Walishangazwa pia na hekima na uwezo mkuu wa Wanafunzi wake!
Matendo ya Mitume 4:13
[13]Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
NJIA NA NAMNA SAHIHI YA KUWA ZAIDI YA BINADAMU WA KAWAIDA.
Makala hii, ni maalumu Kwa wenye kiu na njaa ya kuishi maisha ya kiwango Cha juu zaidi ya ubinadamu wa kawaida, (Impacting lives, societies and thoughts) Bila kutegemea visaidizi hatarishi Kwa Afya ya Roho, akili na mwili. (Bila kutegemea Nguvu za giza) fedha, Madaraka ya kimwili au ushawishi mfu.
Mfano rahisi!👇
👉Kitu pekee kinachoweza kuzitofautisha computer mbili zinazofanana Kwa muundo na Kila kitu, yaani (Factory settings) ni software na Applications! Baada ya mtu kununua computer mpya huamua aweke, ku "in-store" Nini na Kwa FAIDA ipi. Wote mnaweza kumiliki Toshiba au HP, zenye uwezo sawa, lakini softwares mkaweka za tofauti, eventually computer Moja inaweza kuonekana janja zaidi kuliko Ile nyingine, japo Zinafanana!!
😁Kwa sababu hiyo, binadamu tutaendelea kufanana, ki maumbile ya kibinadamu tu, lakini viwango vya maisha itasalia kuwa tofauti sana!
SIRI YENYEWE.
Kwa kawaida Kila kiumbe hai hutokana na kiumbe hicho. (Mbuzi atazaa mbuzi, na mtoto wa mbuzi ataitwa mbuzi, au mwanambuzi)
WATOTO WA MUNGU NI MIUNGU WATU!!!
Binadamu anayetambulika katika Ufalme wa Mungu, Yaani raia Halali Kwa Mungu, ni mfano wa Mungu, ni mwana wa Mungu na ni mungu 🤣😂
👉 Kivipi? Mungu aliumba mtu Kwa sura na mfano wake!
Mwanzo 1:26-27
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa MFANO wetu, kwa SURA yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu nchi.
[27]Mungu akaumba mtu kwa MFANO wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
👉Wivu wa shetani uliwaka, baada ya kumwona binadamu kaumbwa Kwa upendeleo maalumu, Yaani Kwa sura na mfano wa MUNGU. Ndipo alipoamua kuwahadaa Hawa na Adamu, (miungu) wasiojitambua, na matokeo yake yakapoteza sura na mfano wa Mungu.
👇
Mwanzo 3:4-5
[4]Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
[5]kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
👉JINSI GANI UNAWEZA KUWA ZAIDI YA BINADAMU?
Uasi wa kwanza ulimwondolea binadamu sura na mfano wa Mungu! Hata hivyo sura na mfano wa Mungu hurejeshwa Tena Kwa wale tu wanaomwamini Bwana Yesu!
Warumi 3:23-24
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
Being justified freely by his grace through the redemption that is in Christ Jesus:
Cha kwanza kabisa, ni wewe kumwamini na kumpokea Bwana Yesu, ili awe Bwana na mwokozi wa maisha yako!
👇👇👇
Yohana 1:12-13
[12]Bali wote waliompokea (Yesu) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
[13]waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
👉Kwa sababu hiyo, siyo Kila binadamu ni mtoto wa MUNGU, Bali mtoto halisi wa Mungu ni yule Aliyezaliwa upya Kwa kumwamini Yesu na kubatizwa katika Roho Mtakatifu!
👉 Watoto wa Mungu ni wale tu waliokubali kuongozwa na Roho Mtakatifu!
Warumi 8:14
[14]Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
👉Hawa ndiyo wale wanaofananishwa na Yesu, mwana wa Mungu!
Warumi 8:29-30
[29]Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
[30]Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.
👉Sisi ni nakala halisi ya Bwana Yesu Ulimwenguni.
1 Yohana 4:17
[17]Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
👉Kama alivyo, ndivyo tulivyo! Yeye tangu mwanzo alikuwa na asili ya Mungu, na hapo ndipo uungu wa watoto wa Mungu ulipo.
Wafilipi 2:6
[6]ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho.
WATOTO WA MUNGU NI VIUMBE VIPYA, SIYO WATU WA KAWAIDA TENA!
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
👉 Huyu kiumbe kipya, siyo yule mwanadamu unayemjua wewe! Ni mtu na nusu, ni zaidi ya binadamu na ubinadamu wenyewe, Kwa sababu ameubwa si Kwa namna ya kibinadamu, Bali kaumbwa Kwa namna ya Mungu.
Waefeso 4:24
[24]mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
FIKIRIA MAISHA YA MTUME PAULO.
Mtume Paulo, kabla ya kumwamini Yesu na kupokea kipawa Cha Roho Mtakatifu, hakuwa na jipya la maana, zaidi ya kufanya ukatiri na kuua watu. Lakini baada ya kufanyika kuwa mtoto wa Mungu na kuwa kiumbe kipya (Dude) ilikuwa hivi 👇👇
Matendo ya Mitume 19:11
[11]Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
👉Mungu hawezi kufanya miujiza, Kwa mikono ya binadamu wa kawaida/dhaifu, Mungu hufanya Kazi Kwa mikono wa watoto wake (miungu)
Binadamu Hawa (miungu) hawaabudiwi Wala kutukuzwa, Kwa sababu wao siyo Mungu, Bali ni miungu tu, wenye kutwaa sura, mfano na asili ya baba Yao!!
👉Kwa kumdhania mtume Petro ni Mungu, watu wengine walitaka kumwabudu!
Matendo ya Mitume 10:25-26
[25]Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, AKAMSUJUDIA
[26]Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni MWANADAMU.
👉Ndiyo, ni mwanadamu lakini Kwa Nini Kornelio anatamani kumwabudu? (Anaonekana siyo wa kawaida)
👉Paulo alipiga Injili, mpaka watu wakaona huyu siyo mwanadamu wa kawaida ni mungu Kwa mfano wa mwanadamu kashuka!!
Matendo ya Mitume 14:11
[11]Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.
👉Watu Hawa walipoziona Kazi za kina Paulo na Barnabas, waliamua kuwaabudu kabisa na kuwatolea sadaka, lakini Paulo anasisitiza, wao ni wanadamu hawapaswi kuabudiwa kamwe! Lakini Kwa Nini watu Hawa wafikirie kuwaabudu?? (Viwango vya maisha ya juu, zaidi ya ubinadamu)
YESU ALIFUNDISHA UKWELI HUU KINAGANAGA!
👉Kuna mtu Hapa anaweza kupaniki, na kudhani pengine nafundisha mambo mapya ambayo hayapo!! au kudhani labda nafundisha mambo ya Zumaridi Edward Bundala 😁😁😁🤣🤣
Pole sana ndugu, haya mambo yamefundishwa tangu enzi za agano la kale mpaka kipindi Cha Yesu, pia MITUME waliyagusia!
Yohana 10:34-36
[34]Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
[35]Ikiwa (Mungu) aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
[36]je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
👉Wayahudi waliponusa harufu ya fundisho hili, kutoka Kwa Yesu walikasirika sana, ikabidi Yesu awakumbushe kuwa siyo jambo wala fundisho jipya! Hata torati waliyokuwa wanadai wanaishika imefunua ukweli huo😂🤣
Wapi huko??
Zaburi 82:6-7
[6]Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
[7]Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
👉Sijui unaelewa?? Mungu anawaita watoto wake miungu, Tena Wana wa aliye juu, lakini anawaonya, wazi kabisa kwamba wasipojitambua na kulijua Hilo, watakufa kama wanadamu wa kawaida!!
MUNGU MMOJA, MIUNGU MINGI!
Ukweli ni kwamba, Mungu ni mmoja tu, lakini miungu ni MINGI, maana watoto wa Mungu katika Ufalme wa Mungu ni wengi pia, hao Ndiyo miungu!!
1 Wakorintho 8:5-6
[5]Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi;
[6]lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.
TABIA ZA WANA WA MUNGU/MIUNGU SIYO ZA KIBINADAMU!!
👉Zipo tabia nyingi mbaya, japo huhesabika kama mambo ya kawaida ya ubinadamu! Sasa Hawa Wana wa Ufalme, ambao Kwa asili ni miungu, huzishinda tabia mbaya hizi, ambazo biblia inazitaja kama tabia za kibinadamu, ambazo mwana wa Mungu hapaswi kuwa Nazo maana yeye siyo mwanadamu wa kawaida!!
Soma hapa Kwa utulivu!!
👇👇👇
1 Wakorintho 3:3-4
[3]kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya KIBINADAMU?
[4]Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
👉 Umeona kitu hapo☝️
Paulo anawashangaa wakristo wa kanisa la Korintho, Kwa Nini wanaonyesha tabia dhaifu za kibinadamu? Hii inamaanisha kwamba, walipaswa wawe juu ya udhaifu wa kibinadamu!
👉 Kumbuka makazi ya wanadamu ni duniani, lakini Kwa Wana wa Ufalme wa Mungu japo wanakaa duniani lakini wao siyo wa duniani!
Yohana 17:14-16
[14]Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
[15]Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
[16]Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
USHUHUDA WA SAMSON
Samson, alifahamu wazi kabisa kwamba yeye siyo binadamu wa kawaida! Kwa kutambua Hilo aliishi Kwa kufuata miiko maalumu Ili asalie kuwa (mungu) kuishi zaidi ya ubinadamu wa kawaida!! Aliishi hivyo na alifanya mambo zaidi ya uwezo wa kibinadamu mpaka alipoasi.
Waamuzi 16:17
[17]Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, NITAKUWA KAMA WANADAMU WENZANGU.
👉 Zingatia sana nilipoandika Kwa herufi kubwa! Samson was an extraordinary man, aliishi zaidi ya ubinadamu, Nini Siri yake? Roho wa Mungu alikuwa ndani yake, Wala siyo wingi an urefu wa nywele zake!
UFALME WA WAFALME, MUNGU WA MIUNGU, BWANA WA MABWANA
👉 Ufalme wa Mungu, tofauti na falme nyingine, wenyewe ni Ufalme wa WAFALME! Kuna Mungu wa miungu na yupo Bwana wa MABWANA!
👉Hii inamaanisha, hakuna mnyonge Wala dhaifu Kwenye huu Ufalme!
Ufunuo wa Yohana 21:27
[27]Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho KINYONGE, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
☝️☝️ Ufalme wa Mungu, ni Ufalme wa Nguvu, siyo wa watu dhaifu! KINYONGE hakina nafasi.
Ufunuo wa Yohana 17:14
[14]Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni BWANA wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Yesu Kristo, ni Bwana wa mabwana na ni mfalme wa WAFALME!
👇👇👇
Ufunuo wa Yohana 19:16
[16]Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
👉Ndiyo maana, hata wanaouingia, Ufalme huu siyo wanyonge, ni watu wenye Nguvu tu!
Mathayo 11:12
[12]Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
👉HUO NDIYO MZAO MTEULE, NA UKUHANI WA KIFALME!
1 Petro 2:9
[9]Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
☝️☝️
Taifa la Mungu👇👇
Waebrania 12:22-23
[22]Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
[23]mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
#Umebarikiwa milele.
Kama una kiu na shauku ya kuwa "Dude" au "mungu" Mimi ndugu yako, nakukaribisha sana katika Ufalme wa Mungu! Katika Ufalme huu, utafanyika kuwa, bwana, mfalme na mungu!!
Kumbuka.
#shetanianaogopamtuanayejuakitu