Unatoa sadaka lakini haufanikiwi jibu hili hapa

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Habari zenu wapendwa

Kumekuwa na mahubiri mengi kwa sasa kuhusu utoaji huko makanisa ata yale makanisa yanaendeshwa kitaasisi lakini nayo mahubiri yao kwa sasa yamehamia zaidi utoaji wa sadaka. Swali Je ? kuna tatizo kuwa wingi wa mahubiri haya makanisani Jibu ni hapana!

Hakuna shida kanisa kuwa na sadaka nyingi mana sadaka zote lengo kubwa ni kurudisha mahusiano na Mungu ambayo tuliyapoteza baada ya wazazi wetu Adam na eva kufanya dhambi pale kwenye bustani ya eden ukisoma kitabu cha mwanzo utaona namna ambavyo binadamu ndiye aliyepewa mamlaka na utajiri wa dunia hii lakini baada ya kufanya dhambi alipoteza mamlaka Ile

MWANZO 1:26
"Kisha Mungu akasema, Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.”

hivyo basi binadamu tunavyomtolea Mungu sadaka tunakuwa tunamtafuta Mungu ili aturudishie mamlaka ile ambayo wazazi wetu Adam na eva waliipata walipokuwa katika bustani ya eden sadaka ni njia ambayo Mungu aliamua kuweka maagano na binadam pale ambapo watafanya dhambi kulikuwa na sadaka nyingi sana ukisoma katika agano la kale lengo ilikuwa ni kurudisha upatano na mahusiano mazuri kati ya binadamu na Mungu

MAMBO YA WALAWI 23:37
Sikukuu za BWANA ni hizi, ambazo mtazipiga mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mmsongezee BWANA sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu, na sadaka za kinywaji, kila sadaka kwa siku yake;

Ukisoma kitabu cha mambo ya walawi utaona jinsi ambavyo sadaka zilivyokuwa ni nyingi ikiwa mtu umefanya dhambi au ikiwa mtu anataka baraka kwa Mungu kulikuwa na sikukuu za vibanda Wana wa Israel walikuwa wakikutana kila baada ya miezi saba kwa mwaka lazima wakutane siku saba kwaajili ya kumuabudu Mungu na kutolea sadaka na dhabihu kwa ambao hawatotoa sadaka basi watakutana na laana na magonjwa

ZEKARIA 14:18
"Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda.

Katika baadhi ya sadaka na sikukuu hizo zilitolewa kama kivuli cha Bwana wetu Yesu Kristo hapa anatufundisha mtume paulo katika

WAKOLOSAI 2:16-17
mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Kama nilivyosema hapo juu bado hakuna tatizo ya kuwa wingi wa sadaka hata sasa wingi wa sadaka nikutokana na watu kuendelea kufanya dhambi ni kama vile mgonjwa kazidiwa zaidi atahitaji dozi kubwa zaidi kumtibu hivyo sadaka kuwa nyingi ni matokeo ya binadamu kuwa mbali sana uwepo wa Mungu hivyo anahitaji kurudisha mamlaka Ile kwa kumtolea Mungu sadaka

Turudi kwenye mada yetu kwanini mtu anatoa sadaka lakini anazidi kufirisika au hapati baraka jibu ni hili sadaka Ile ilikuwa inatolewa kipindi cha walawi sio sadaka ya sasa ambayo ili ubarikiwe ni lazima uongozwe na Roho Mtakatifu maono haya ya kujazwa kwa Roho Mtakatifu kwa kila aaminiye ilitabiriwa hata kabla ya kuja kwa Yesu

Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu, ubora na ushawishi wa Mungu juu ya ulimwengu au viumbe vyake.
Kama unataka kubarikiwa jambo fulani unataka kupona ni lazima uongozwe na Roho Mtakatifu akuongoze ni sadaka ipi itakuhitaji uindalie fungu la kutosha ukiwa na Roho Mtakatifu ni lazima utakuwa na kipaumbele na sadaka na unayoenda kumtolea Mungu ili aachilie baraka ila ukiongozwa na mwili utaishia kutoa sadaka bila matokeo unayoyataka
Utoaji wa sadaka ni kama vile ambavyo umeona dalili ukaenda kwa daktari akakupima akakuandikia dawa mbili au tatu zote zinatakiwa lakini wewe utakuwa umejua dawa ipi inaenda kumaliza tatizo lako moja kwa moja Dactari hawezi kukuandikia dawa bila vipimo hata katika utoaji wa sadaka bila msaada wa Roho Mtakatifu huwezi jua ni sadaka ipi itakubariki,itakuponya au itakuondokoa katika magumu unayopitia wewe utatoa tu sababu nabii amekuambia ukitoa sadaka utabarikiwa
Makanisani Kuna sadaka nyingi Kuna sadaka za zaka,malimbuko, ujenzi,mavuno kuchangia watoto yatima, nk. zote ni zinakuhitaji ila wewe ukiongozwa na Roho Mtakatifu utakuwa umeshajua sadaka ipi inayoenda kumaliza tatizo kabisa uwe una kesi inakwenda kuisha, magonjwa yote yanapona,baraka zinakufuata hakuna kinachokosa majibu katika hayo yote mana kila jambo Lina majibu ukiwa na zawadi ya Roho Mtakatifu ndani yako

Ata usomaji wa biblia ukiongozwa na Roho unaenda kutatua matatizo yote
Usikilizaji wa nyimbo za injili ukiongozwa na Roho unabarikiwa

Hakuna anaeyeweza kuomba impasavyo Mungu bila kuongozwa na Roho Mtakatifu inatuthibitishia hapa katika kitabu cha

WARUMI 8 26
Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno

Wahubiri wengi kwa sasa hawawaandai kondoo wao katika mahubiri ya kuwakuza kiroho mahubiri mengi imekuwa toa ubarikiwe mwisho watu wamekuwa hawapati matokeo sababu kutomtambua huyu Roho Mtakatifu anafanyaje kazi

wakati Yesu anawaacha mitume wake anapaa kwenda mbinguni alimuomba Mungu awape mitume wake msaidizi mwingine ambaye ni Roho mtakatifu kwahiyo hawa mitume ndio wakwanza kupokea Roho mtakatifu maana ulimwengu haukujua chochote kuhusu chochote zawadi hii ya Roho mtakatifu kwahiyo walipewa Roho Mtakatifu ili nawao waendee ulimwengu mzima wakahubiri injili ili watu wampokee Bwana Yesu na wakafundishe ili watu wabatizwe kwa Roho

YOHANA 14:17
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Asanteni sana mbarikiwe wote mtaosoma andiko hili

Asanteni mbarikiwe sana wote mlioosoma andiko hili
 
Kabisa bila kupata ushauri wa Roho Mtakatifu mta anaweza kufanya kila kitu lakini asifanikiwe kabisa, ukipata maarifa ya Roho Mtakatifu kufanikiwa ni mara moja tu.
 
Nipeni namba za Mungu nimtumie sadaka kwa mpesa directly.
Ukisaidia mwenye uhitaji utakuwa umemtolea Mungu lini ulienda kuangalia wagonjwa na kuwapa ata maji ama uwa unaenda hospital mpaka uwe na ndugu anaumwa
 
Back
Top Bottom