Unatumia fridge ipi kati ya hizi?

Koffi Annan

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2018
Posts
1,771
Reaction score
5,087
Fridge zipo za aina tofauti kulingana na ujazo na aina ya matumizi, fuatana nami katika Makala hii fupi itakayokuongoza namna ya kuchagua kulingana na mahitaji yako;

Fridge zenye pande mbili
Hizi ni fridge zenye nafasi kubwa kuliko zote, zinafaa kwa matumizi ya familia au kwa wewe mwenye mamisosi ya kumwaga, nyingi zinakua na upande mmoja freezer kugandisha na mwingine fridge kwa ubaridi wa kawaida. Kuna zenye water dispenser na zingine hazina.
Hizi zinaanzia 1.8M-7M kulingana na ujazo na kampuni.

Fridge za milango wa juu na chini, hizi zinakua na freezer upande wa juu (Top Freezer) na (Bottom Freezer); Utatumia Top Freezer kwa matumizi ya kawaida na Bottom freezer kama unahitaji freezer kubwa kwa ajili ya kugandisha hasa kama unanunua vitoweo kama nyam ana Samaki stock nyingi.
Hizi zinaanzia 700K-2.5M kulingana na ujazo na kampuni.
Bottom Freezer inakua na freezer upande wa chini ambayo huwa kubwa sana kuliko Top Freezer
Top Freezer
r
Bottom Freezer

Fridge ya mlango mmoja hizi zinafaa sana kwenye single rooms zinakua na nafasi nzuri kwa matumizi madogo, na zipo ndogo kabisa ambazo unaweka chumbani kwa ajili ya matumizi binafsi. Hizi zinaanzia 300k-1M kulingana na ujazo na kampuni.





TRENDING FRIDGES

Teknolojia ya fridge nayo inakua kama zilivyo electronics nyingine, Samsung Mirror fridge na LG Instaview ndio fridge za kisasa kutoka kampuni mbili zinazoongoza kwa ubora kwa bei ya 5/6Million;


Matumizi madogo ya umeme, nafasi kubwa, water dispenser yenye ice maker na rangi tofauti ni features zilizopo kwenye fridge nyingi za kisasa.Fridge za kisasa hazigandishi barafu kwa ndani, zina feature ya kutoa harufu ya vyakula inakuwa inanukia fresh muda wote ukifungua, lakini pia zinatumia umeme kidogo.

Kampuni za Samsung, Westpoint, LG na Hisense ndio fridge zinazokimbiza kwa soko la bongo ila kampuni zote za electronics zina fridge tofauti, ukishindwa bei kati ya hizo nilizotaja jaribu kampuni nyingine za kachina ambazo zina bei ya chini, huko unapata fridge yenye pande mbili mpaka kwa 1.5M.

Uliza swali lolote linalohusiana na fridge, bei, aina/kampuni, ubora, matumizi na matengenezo.
 
Ni kweli fridge guard muhimu kwenye fridge? Na je unaweza kuitumia na kwenye TV?
 
Mkuu vipi zile fridge za biashara ya samaki za kioo bei yake?
 
Chest freezer ikoje yenyewe.
Pia nahitaji freezer ya kwa ajili ya ice blocks niwauzie wauza vinywaji pamoja na wauza samaki na pia hata mtu uweze kutengeneza barafu za kuuza za shilingi mia mia ama hamsini.

Pia utajuaje uwezo wa freezer Kuna moja hapa niliiona imeandikwa freezing capacity 18kg/24hrs inamaanisha nini hiyo hapo juu
nielezee hii kidogo ikoje,
 
Ni kweli fridge guard muhimu kwenye fridge? Na je unaweza kuitumia na kwenye TV?
Kuna fridge zina inverter, moja ya kazi yake ni power stabilizer hivyo sio lazima kutumia guard; kampuni kubwa ndio zina fridge zenye inverter compressor, za kichina nyingi hazina
Fridge guard unaweza kutumia kwenye TV ila ya TV kama ina volts ndogo haitaweza kuendesha fridge,
Stabilizer itatumika kwa zote mbili bila mashaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…