Unatumia mbinu gani kujua ukweli wa taarifa unazokutana nazo mtandaoni?

Unatumia mbinu gani kujua ukweli wa taarifa unazokutana nazo mtandaoni?

1708439365113.jpeg
Kukua kwa utandawazi kumepelekea wimbi la uzwalishwa wa taarifa potofu kuongezeka zaidi licha ya kuwepo tangu awali.

Katika kukabiliana na wimbi hili zipo njia mbalimbali ikiwemo kuhakiki chanzo cha taarifa na kuuliza kwenye jukwaa la uhakiki kama hili la JamamiiCheck.

Huwa unatumia mbinu gani kutambua uhalali wa taarifa unazokutana nazo mtandaoni kabla ya kuziamini?
 
Hakika hili suala la taarifa za mitandaoni bado ni shida kidogo

Wapo baadhi ya watu wanaotumia majina ya watu maarufu katika mitandao ya kijamii kwa malengo yao Binafsi.

Hili ni suala hatari sana na haswa kwa watumiaji wapya wa mitandao hiyo.
 
Mimi kiukweli naendaga kwenye account ya Milard Ayo.. ndo niangalie kama amepost ndo niamini. Ila kwa sikuhiz nimeona sehemu sahihi ni JF.Whatsapp channel
Kwasababu ipo karibu na mahala ninapopenda kuchati. Mahala hapo ni WhatsApp
 
Uhalali naupata kwa kupitia kurasa zilizo rasmi kama JF, Milard Ayo, vyombo vingine vya habari mara nyingine watu maarufu na wenye weredi mkubwa kwenye tasnia ya habari.
 
Huwa unatumia mbinu gani kutambua uhalali wa taarifa unazokutana nazo mtandaoni kabla ya kuziamini?
Kwa kufuatilia vyanzo makini pekee maana hakuna chanzo makini kinachoweza kutoa taarifa za uongo
 
Back
Top Bottom