Unatumia njia gani kuwapata wateja kwenye biashara yako?

Unatumia njia gani kuwapata wateja kwenye biashara yako?

Just_Me

Member
Joined
Mar 12, 2019
Posts
23
Reaction score
22
Nmegundua kwamba sio wafanyabiashara wengi wanatumia mitandao (Internet) kuwapata wateja wao, wakati ukweli ni kwamba kwa kutumia mitandao hasa mitandao ya kijamii unaweza kuwapata wateja wengi kwenye biashara yako na kukuza soko lako, hii ni dhahiri hata kwa wale wachache waliochagua kutumia mitandao ya kijamii wanaona matunda yake.

Nadhani pengine ni mazoea tu kwamba kwa hali ya kawaida mfanyabiashara wa kitanzania anakua haoni kama anaweza pia kupata wateja zaidi ya wale waliomzunguka mf. Dukani kwake.

Nimeona upo uwezekano wa kutengeneza mfumo wa mtandaoni ambao unaweza kukusogezea karibu wateja kutoka mbali, zaidi ya majirani wako kwenye site ya biashara yako, upo uwezekano wa kufungua duka kariakoo lakini ukawapata wateja kutoka kila kona ya jiji. Lakini pa kuanzia ni kujua ni njia gani unayotumia kwa sasa ivi kuwapata wateja wako? Kama ni matangazo ni matangazo ya aina gani, na kwa nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hutegemeana na aina ya biashara, ya kuuza bidhaa au ya kutoa huduma. Na zote huweza kutumia mtandao kupata wateja ila kuna system ambayobhutumiwa na biashara kubwa ulimwenguni kupata na kuendelea kuwa na wateja na hii hujulikana kama ATM(Acsending Transaction Model)
 
Kuna njia moja ambayo mimi nimeitumia binafsi.

Kuna application inaitwa BULK SMS.

Mfano, waza mesej kutoka makampuni ya simu. Labda wanatangaza ofa mpya, ebola, ujumbe kutoka polisi n.k

Nilivyokuwa nafanya kazi BRANCH ya TIGO ocean road, miaka miwili iliyopita, tulikuwa tunatuma hii meseji kwa wateja.

''Hongera mteja, Tigo imekuchagua kujiunga na kundi la wateja muhimu wa postpaid. Hutasumbuka kununua vocha tena. Kujiunga tembelea duka la tigo au piga simu namba 0755 XXX XXX''

Ndani ya masaa, mamia ya wateja walikuwa wanakuja dukani, kuulizia hiyo meseji ina maana gani. Kuna ambao waliishia kununua product, wengine walikuwa wanataka kujua tu.

Hiyo app inapatikana kampuni yeyote ya simu. Malipo yake yanafanyika kwa mwezi. Na unapewa vifurushi vya kuchagua.

Kuna vya elfu arobaini (meseji 1000), elfu hamsini na kuendelea. SIFANYI kazi kampuni za simu tena. Sasa hivi nimejiajiri.

Hiyo app inaleta matunda, kama bidhaa yako inalenga MATATIZO ya watu. Ukilenga tatizo, na ukatoa SULUHISHO, wateja watakuja.

Ni mojawapo wa mbinu. Siyo mbinu pekee.
 
Nadhani mbinu kubwa nowadays ni kufanya digital marketing kupitia social media. Jua namna ya kudesign na kuvutia wateja, nimewatengenezea wengi matangazo na wamefanikiwa pia. Vile vile pia hakikisha bidhaa yako pia umeifanyia branding nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wengi mnamwaga madini kwa biaahara za mjini tu, ebu tufikirieni na sisi wa huku Ibadakuri, Mwendakulima shinyanga au Mundarangavye, kimilamila, Gwachokora na Mwibambo Kagera ambako wateja ma wanachi wengi hawana smartphones wala. hajui uwepo wa pc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza ukatumia njia mbali mbali:

-Nenda door to door. Au nyumba kwa nyumba ukiuza bidhaa yako

-Weka meza kwenye soko, au barabarani. Fanya ''demo'' kwa kutumia microphone ku-promote bidhaa yako. Kuna ambao watajipitisha ili kujua unasema nini. Lenga wanawake.

-Tengenza vipeperushi, au mabango madogo, yabandike ukutani, kwenye nguzo za umeme, kwenye nyumba za watu n.k...

-Omba wateja ulionao wakuunganishe na wateja wengine

-Mwambie mteja, utampa bidhaa moja bure pale mteja atakaponunua zaidi ya mara tatu...Hii mbinu itamfanya AWAAMBIE wenzake

-Fungua duka eneo ambalo linamzunguko kidogo
 
Back
Top Bottom